UVCCM: Rais Magufuli Amefanya Mambo Makubwa Katika Miaka Mitatu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWImJhgdD-JPt7aR3tOD1cT7frrFoRK7DEZa2G26B1384wrZh8oBlb5GYkSn4q4XPtWggmTlOvaiE41MZmUhyphenhyphenXxsl2ApViNnAgjAa6chJQJ2PtmjGSLwAYWruQrxIFigPKrDiIUJW11zHQ/s640/Screenshot_20181224-222953%257E4.png)
Wananchi wametakiwa kuendelea kumwunga mkono rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hili aweze kutekeleza majukumu yake na kuwaletea maendeleo ya kweli nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Uvccm taifa Mwalimu Raymond Mwangala Alisema kumekuwepo na propaganda kutoka kwa baadhi ya watu na viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa nchini kupotosha ukweli kwa hatua ambazo amekuwa akizichukua rais magufuli wakati alitekeleza majukumu yake.
"Mpaka sasa Serikali ya CCM chini ya Rais Dk. Magufuli imefanya utekelezaji mkubwa wa mambo mbalimbali ya maendeleo yanayogusa moja kwa moja maslahi ya mapana ya wananchi ambayo yameainisha katika Ilani ya CCM 2025-2020,” alisema Mwl. Mwangwala.
Mwangwala alieleza kuwa serikali imeweza na inaendelea kusimamia utekelezwaji wa miradi mbalimbali mikubwa ambayo itasaidia kufikia uchumi wa kati.
Alitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), Ujenzi wa Flyover ya Tazara kwa Mfugale, Ujenzi wa Daraja la Salender, Ujenzi wa Barabara ya Njia Nane kutoka Kimara-Kibaha.
Mingiine ni Mradi wa Umeme Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Hydropower Dam), Elimu Bure, Ununuzi wa Korosho na Ununuzi wa Ndege.
Akizungumzia ndege iliyoingia nchini jaana Desemba 23, 2018, alisema ni ya kwanza kwa nchi za Afrika hivyo kila mtanzania anatakiwa kupongeza juhudi za Rais Magufuli za kuliimarisha Shirika la Ndege la ATCL.
Kutokana na jitihada hizo, alitoa wito kwa Watanzania kumsaidia Rias kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta maendeleo.
Aidha alisema kama UVCCM wapo tayari kumlinda, kumtetea na kumpigania Rais Magufili ili kuhakikisha anafikia adhima yake yakuhakikisha tunafikia uchumi wakati.
"Vijana wa CCM tutakuwa wa kwanza kumlinda Rais Wetu ili kuweza kufikia uchumi wa kati"
Alisema kutokana na mambo hayo makubwa yaliyofanywa na serikali, UVCCM umeipongeza serikali na kuendelea kuwatia moyo watendaji wake chini ya Rais Magufuli ili kuendelea kushughulika na kero za watu.
No comments