Vijana Changamkieni Mafunzo Yanazotolewa Na Chuo Cha Taifa Cha Utalii Nchini.
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii Tanzania Bi. DEVOTHA MDACHI
akiongea wakati wa ufunguzi wa tamasha
la maonyesho ya la taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Dar es salaam:
Vijana nchini watakiwa kuchangamkia
fursa za mafunzo yanayotolewa na chuo cha taifa cha utalii (NCT) ili
kuwawezesha kuweza kutapa ujuzi ambao utawasaidia kuwapatia ajira sambamba na
kujiajili wa wenyewe.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
tamasha la maonyesho ya la taaluma katika chuo cha taifa cha utalii jijini Dar
Es Salaam kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara ya maliasiri na utalii , Mkurugenzi
mkuu wa bodi ya utalii Tanzania Bi. DEVOTHA MDACHI alisema vijana wajitokeze
kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo zinazopatika mara baada ya kuhitimu mafunzo
ya yjuzi yanayotolewa na chuo hicho.
“Vijana jitokezeni kuchangamkia fursa
zinazotolewa na chuo cha taifa cha utalii kwani zitawasaidia vijana katika kutatua
tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana, sambamba na kuwaongeza kipato hivyo kuinua
uchumi wa nchi kupitia vijana” alisema Bi Mdachi.
Alisema serkali kupitia wizara ya
maliasiri na utalii imetoa gari moja dogo ambalo litawasaidia vijana katika
kufanikisha utalii wa ndani kuunga mkono jitihada za chuo hicho katika
kuendelea kutoa mafunzo yanayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Mwenyekiti Wa Bodi Ya Ushauri Ya Chuo
Cha Taifa Cha Utalii Bi. BENADETA NDUGURU akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo
cha taifa cha utalii (NCT), April 27
2018 jijini Dar Es Salaam.
Kwa upande wa Mwenyekiti Wa Bodi Ya
Ushauri Ya Chuo Cha Taifa Cha Utalii BI. BENADETA NDUGURU alisema wameandaa
tamasha hilo kufatia kutambua umuhimu wa vijana katika kujenga uchumi wa nchi sambamba
na kuwakutanisha wadau kutoka taasisi mbali mbali zinazojishughulisha na utoaji
wa huduma za kupokea watalii, mahoteli, waongoza watalii hili kuweza kujionea
namna chuo hicho kinavyo toa mafunzo yake.
Aidha Bi. Ndunguru aliongeza kuwa kupitia
tamasha hilo wadau wataweza kujionea jinsi chuo hicho kinavyoendesha shughuli
zake hivyo kuwa moja ya njia ya kuwawezesha wahitimu wao chuo hicho kupata
ajira kwa urahisi.
Atamasha hilo ambalo limebeba ujumbe usemao
"FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA TAALUMA YA UKARIMU NA UTALII" ikiwa
kama njia ya kuufahamisha uuma juu ya mafunzo yatolewayo katika chuo cha taifa
cha utalii.
Mkurugenzi wa chuo cha taifa cha
utalii Bi. Sporah Liana akifafanua
jambo katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbali mbali
wakiwasilisha mada katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa
cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini
Dar Es Salaam.
Washiriki tamasha hilo kutoka taasisi
mbalimbali wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika tamasha la maonyesho
ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Mgeni rasmi katika tamasha la maonyesho ya la taaluma Bi. DEVOTHA MDACHI akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wakati alipotembelea mabanda ya wanafunzi hao kujionea namna shughuli zinazofanywa na kuratibiwa na chuo hicho katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Washiriki wa tamasha hilo wakifatilia
kwa makini mada ambazo zikiwasilishwa katika tamasha la maonyesho ya taaluma
katika chuo cha taifa cha utalii (NCT),
April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Mgeni rasmi katika tamasha la maonyesho
ya la taaluma Bi. DEVOTHA MDACHI akiwa katika picha ya pamoja na vingozi wa
chuo icho pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika tamasha la maonyesho
ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
No comments