Tume Ya Uchaguzi (NEC) Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Kuhusu Uhamisha Vituo Jimbo La Kinondoni
Na Hussein Makame,
NEC
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imesema uamuzi wa kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika jimbo la
Kinondoni umezingatia matakwa ya kanuni za Uchaguzi kwa kuvishirikisha vyama
vyote vya siasa ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani jijini Dar es Salaam, kufuatia
taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya magazeti zinazodai kuwa Chadema
hakikushirikishwa katika uamuzi wa kuhamisha vituo hivyo.
Alisema kabla ya
uamuzi wa kubadilisha vituo hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni
iliitisha mkutano na vyama vya siasa tarehe 30 Januari, 2018 na wawakilishi 26
walishiriki kwenye mkutano huo wakiwemo wawakilishi wa Chadema.
“Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kwa kushirikiana na vyama vya siasa katika kikao kilichofanyika tarehe
30 mwezi Januari mwaka huu walikubaliana kuhamisha vituo 46 na katika vituo
hivyo vituo 16 viko kata ya Kigogo, vituo 8 viko kwenye kata ya Mwananyamala na
vituo 22 viko kwenye kata ya Kijitonyama” alisema Kailima.
Alifafanua kuwa
kwa mujibu wa kifunga cha 21 (1) cha kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura, vituo vya kupigia kura havitakiwa kuwa kwenye maeneo ya watu
binafsi, nyumba za mashabiki wa vyama vya siasa au maeneo ya majeshi na ibada.
“Nimesikitishwa na
kauli ya Chadema eti hawakushirikishwa, nimesikitishwa kwa sababu kumbukumbu za
mikutano zilizopo tarehe 30 Januari mwaka huu, chama cha Chadema kiliwakilishwa
na Mwenyekiti wa Wilaya Bw. Mustafa Muro pamoja na Katibu wa Wilaya Bw. Shabani
Kirita” alibainisha Kailima.
Alifafanua kuwa
wawakilishi hao walihudhuria mkutano wa msimamizi wa Uchaguzi jimbo la
Kinondoni na vyama vya siasa na katika mkutano huo kulikuwa na ajenda moja tu
kuhusu kuhamisha vituo vya kupigia kura na vyama vyote kwa pamoja vilikubaliana
kikiwemo Chadema.
“Unaposema chama
cha Chadema hakikuhusishwa ninapata masikitiko makubwa sana.Tume ya Taifa ya
Uchaguzi haiwezi kuingilia mawasiliana ya ndani ya chama husika, kwa hiyo kama
hakuna mawasiliano kati ya makao makuu na ngazi ya Wilaya hilo sio tatizo la
Tume” alisema Kailima.
Alifafanua kuwa
katika kata ya Kigogo kuna baadhi ya vituo vya kupigia kura vilikuwa ndani ya
msikiti wa Kigogo na vingine vilikuwa ndani ya eneo la Zahanati eneo ambalo
lilikuwa dogo kutosha kwa ajili vituo vya kupigia kura.
Kailima aliongeza
kuwa, vituo 8 vya Mwananyamala vilikuwa kwenye eneo ambalo wananchi walikuwa
wanalilalamikia, vyama vya siasa vikaridhia kwamba vituo hivyo vihamishwe na
vituo 6 vikapelekwa kwenye kata inayohusika na vituo 2 vikapelekwa uwanja wa
Kopa.
Akizungumzia vituo
22 kwenye kata ya Kijitonyama, Kailima alisema vyama vyote vilikubaliana
kuvihamisha, hivyo Chadema kikisema havikukubaliana ndipo inapoleta shida.
Alisema Maelekezo
kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kipengele cha 9 (2) (C) kinasema kabla vituo vya
kupigia kura havijahamishwa ni lazima Tume ishirikiane na vyama vya siasa na
Tume imetimiza takwa hilo la kikanuni na vyama viliitwa vikakubali.
“Ukisema huwezi
kuhamisha vituo kabla hujafanya Uboreshaji, huwezi kuacha makosa yakaendelea
kuwa makosa.Hatujahamisha kutoa mkoa mmoja kwenda mwingine, bali tumehamisha
kwa ridhaa na vyama vikaridhia.
“Kwa hiyo niwasihi
chama cha Chadema kabla hakijaanza kulaumu wawasiliane na wenzao kwenye ngazi
husika.” Alisema Kailima.
Katika hatua
nyingine, Kailima amelisihi gazeti la Mwananchi, litoe habari sahihi kuhusu
Tume na kuacha kuandika habari zinazoihusu Tume bila ya kuwasiliana nayo
‘kubalance’ kuhusu habari husika.
“Nalisihi gazeti
la Mwananchi, tunaliheshimi ni gazeti bora na gazeti linaloheshimika, lakini
nilisihi kabla halijatoa habari lazima lifanye balance ya habari” alisema
Kailima na kuongeza kuwa:
“Wenyewe
walipowauliza Chadema wakasema hawakushirikishwa walitatakiwa kuchukua fursa ya
kuwauliza Tume kama hawakushirikishwa.
“Kwa hiyo nilisihi
kwa sababu si mara moja wala mara mbili wamekuwa wakitoa taarifa ambazo si
sahihi kuhusu Tume, tunawasihi na kuwaomba wanapotaka kutoa habari za Tume
watoe habari za Tume zikiwa sahihi”
Alifafanua kuwa
kulitaka gazeti hilo kwamba hata linapotaka kukosoa ni lazima likosoe kwa
habari sahihi na sio kwa habari za upotoshaji na za upande mmoja.
No comments