Mjadala Wa Sakata La Msamaha Wa Babu Seya Waibukia Bungeni
Mbunge wa
Temeke kwa tiketi ya (CUF) Mhe. Abdalah Mtolea ameibua sakata la kusamehewa
Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza 'Papii Kocha' na kusema halikuwa jambo jema
kwa kuwa watu hao mahakama iliwabaini kuwa ni wabakaji.
Mtolea
amesema hayo jana Februari 7, 2018 akiwa bungeni na kudai kitendo cha watu hao
kuachiwa na kupewa heshima na Serikali ikiwa pamoja na kuwapandisha kwenye
majukwaa mbalimbali na kuwapa ufadhili haileti picha nzuri kwa jamii.
"Kwenye
maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ukatoka msamaha kwa Babu Seya na wenzake
watu ambao pasipo na shaka mahakama zilithibitisha kwamba hawa watu ni wabakaji
sasa tunapokuwa tunasamehe wabakaji uko wapi ulinzi wa watoto wa taifa
hili,tunawapandisha kwenye majukwaa wafanye show yaani tunawaona kwamba ni kioo
cha jamii je wanafundisha nini? Alihoji
Mhe.
Mtolea aliendelea kusema kuwa "Je, mnataka kwamba siku ya mwisho
tukiwauliza watoto ukiwa mkubwa unataka kuwa kama nani aseme nataka kuwa
mbakaji?
Babu Seya
na mwanaye Papii wanategemea kuachia kazi yao mpya muda si mrefu baada ya
kuiaanda mara tu baada ya kupewa msamaha na Rais John Pombe Magufuli
No comments