Breaking News

Diwani SONGORO MNYONGE: Mkichagua Mtulia Kinondoni Nitashirikiana Nae Kutatua Kero Zinazowakabili.

Image result for Diwani wa kata hiyo mh. SONGORO MNYONGE
Na Sala Mlawas
Halmashauri ya manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam katika kata ya mwananyamala imetakiwa kutengea bajeti ya kiasi cha shilingi milioni 650 zitakazosaidia kufanyika ujenzi wa mifereji mikubwa ambayo inapelekea adhari kwa wananchi wa kata hiyo.

Akizungumza na wakazi wa kata hiyo jijini dar es salaam na Diwani wa kata hiyo mh. SONGORO MNYONGE alisema wananchi wengi wanakumbwa na mafuriko Mara kwa Mara kwani kero hizo zinatokana na mfereji huo kuwa na kina kidogo kinachoshindwa kumwaga maji baharini.

Alisema kutokana kuwepo na changamoto hiyo ambayo imekuwa ikijitokeza Mara kwa Mara hususani katika mitaa ya MSISIRI A na B hivyo kuwataka wakazi wa mtaa huo kumchangua Mgombea Ubunge wa ccm Bwana Maulid Mtulia watashirikiana nae bega kwa bega kuhakikisha wanalipatia suluhu tatizo hilo.

Aidha Mhe. Mnyonge alisema tayali takribani kaya 12 zilizopisha mradi wa DMDP na ujenzi wa barabara wametengewa bajeti yao na watalipwa hivi karibuni hili mradi huo uanze kutekelezwa.

Kwa upande wake  Katibu wa Itikadi na Mwenezi CCM Taifa Bw.Hamphrey Polepole ameitaka Halmashauri ya manispaa ya kinondoni kutenge milioni 30 mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi wa Pili kwa ajili ya wajasiliamali wa kata ya mwananyamala .

Bw. Polepole alisisitiza kuwa fedha hizo ambazo zinatalenga Vijana na akina Mama katika sekta ya kuleta maendeleo nchini.

No comments