Atupwa Jela Kwa Kumwekea Mkewe Pilipili Kwenye Chupi....Sehemu Za Siri Zikavimba
Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la
Moses Okello amehukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi za jamii kwa siku 40,
baada ya kukutwa na hatia ya kumtilia pilipili mke wake kwenye nguo ya ndani
'chupi'.
Mke wa Okello aliiambia mahakama kuwa
mume wake huwa anapenda akiwa amevaa nguo hiyo, na siku hiyo alimlazimisha sana
kuivaa na kutekeleza, na baada ya muda mfupi alihisi kuwashwa na kuvimba sehemu
za siri na kuamua kwenda kumuona daktari, ndipo walipogundua ilikuwa ni
pilipili.
“Aliniambia anavutiwa sana na mimi
nikiwa nimevaa hiyo nguo akawa ananilazimisha kuivaa, baada ya kuivaa nikaanza
kuhisi muwasho sana, nikaenda kumuona daktari na kugundua ilikuwa pilipili”,
amesema Mke wa bwana Okello ambaye jina lake limehifadhiwa.
Moses alikiri kufanya tukio hilo kwa
mkewe, na kusema kwamba ulikuwa ni utani ambao amezoea kufanyiana na mke wake
huyo kipenzi.
No comments