Kigogo Wa Escrow Aachiwa Huru
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuachia huru aliyekuwa
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea
rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya
zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Esrow.
Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amemuachia huru Rugonzibwa leo Alhamisi baada
ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kesi hiyo
iondolewe mahakamani hapo chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Makosa ya
Jinai (CPA) na Mahakama kuridhia.
Rugonzibwa
alifikishwa na Takukuru mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 14, 2015
akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa Rugemalira
fedha ambazo ni sehemu ya zile Akaunti ya Tegeta Esrow.
Hata
hivyo baadaye alibadilishiwa hati ya Mashtaka na kusomewa upya ambayo
hayakuonyesha tena kuwa fedha zilizopokelewa na Mujunangoma toka kwa Rugemalira
ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kupitia
hati hiyo mpya, Rugonzibwa alikuwa akidaiwa kuwa Februari 5, 2014 akiwa
mtumishi wa Serikali kama Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipokea rushwa ya Sh Sh323 milioni kupitia
akaunti yake namba 00120102602001 iliyopo kwenye Benki ya Mkombozi .
Alidaiwa
kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rugemalira, ambaye ni mshauri
huru wa kitaalamu, mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya
Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa
kampuni hiyo.
Baada ya
kusomewa mashtaka hayo, alikana na upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekwisha
kamilika.
No comments