Amref Yazindua Mradi Wa Hamasa Katika Uzazi Wa Mpango Mikoa 24 Nchini.
Hali ya uzazi wa
mpango nchini bado ni changamoto kubwa kutokana na asilimia kubwa ya wananchi
hususani waishio vijijini kuendelea kuzaaa idadi kubwa ya watoto huku kipato
chao ni kidogo hali ambayo inawafanya washindwe kuwahudumia.
Akizungumza mapema
leo Jijini Dar es salaa, Mkurugenzi wa Amref helth Africa Dkt. Frolence Temu mara
baada ya hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa health Systems Advocacy ambao una
lengo la kuhamasisha jamaii kutambua namna ya kupanga uzazi pamoja na faida
zake.
Dkt.Temu alisema
mradi huo ambao unadhaminiwa na serikali ya Uholanzi kwa euro milioni 150 na unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu katika
mkoa wa SHINYANGA kutokana na mkoa huo kuwa na changamoto kubwa ya wananchi
kuzaa watoto wengi nakushindwa kuwa patia Huduma za msingi kama vile chakula, malazi.
Mapema akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Afya ya Uzazi wa Mtoto Bw. Machumu
Miyeye ambaye ni Mfamasia kitengo cha Afya ya uzazi na mtoto alisema serikali
inaendelea kuchukua hatua za makusudi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa
kutoa elimu juu ya uazi w mpangoili kukabiliana na ongezeko la idadi ya watu nchini.
Kwa upande wake
Meneja Miradi ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa Dkt.Sarafina
Mkuwa alisema mradi huo utatekelezwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kufanya mikitano mbalimbali itakayo wahusisha viongozi kuanzia ngazi za
serikali mitaa pamoja na wananchi.
Aidha amewahakikishia
wananchi kuwa matumizi ya njia za uzazi wa mpango hazina madhara kama baadhi ya
watu wanavyopotosha,nakusema kuwa njia hizo ni salama.
Akitaja baadhi ya
faida za uzazi wa mpango Dr. Mkuwa amesema kwamba inasaidia wakina mama kuwa na
Afya bora,watoto kukua kwa mpangilio mzuri nakusaidia pia familia kuendelea
kiuchimi.
No comments