Dc Wa Temeke Mhe Lyaviva Ataka Uadilifu Zoezi La Usajili Vijana Wanaojiunga Na Jkt
Mkuu Wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva
Na sara Mlawas:
Mkuu Wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva amewataka
madiwani Wa manispaa hiyo kusimamia vizuri zoezi la usajili vijana watakao
jiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) bila kuruhusu kuwepo mianya ya kupokea
rushwa.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es
salaam katika kikao cha baraza la madiwani Wa Manispaa hiyo alisema mtendaji
yeyote atakayebainika kwenda kinyume na utaratibu uziliopangwa katika zoezi
hilo la usajili hatachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi.
“Natoa
wito kwa watumishi wote ambao wanahusika kusimamia zoezi hili kufata sheria na
taratibu wakati wote wa zoezi la undikishwaji yeyote atakayebainika kukiuka
sheria na taratibu zilizopo hatachukuliwa hatua haraka” alisema Dc Mhe.Lyaviva.
Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Abdallah Chaurembo
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Abdallah Chaurembo amemhakikishia Mkuu
Wa Wilaya huyo kuwa utaratibu utakao tumika katika zoezi hilo la usajili ni ule
uliopangwa na manispaa hiyo.
Aidha Mhe. Chaurembo amewataka
madiwani kuhakikisha wanajikita kujadili njia bora za ukusanyaji Wa mapato ili
kuiwezesha maspaa hiyo kuweza kutatua changamoto mbali mbali zinazokabili
Wilaya hiyo.
No comments