Breaking News

Waziri Ummy: Kuongoza Matembezi Ya Hisani 28 oct Kuhamasisha Na Kuchangia Damu Wagonjwa Wa Saratani

Image result for waziri ummy mwalimu
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ataongoza matembezi ya hisani  kuhamasisha na kutoa elimu ya saratani ya matiti na kuchangia damu.

Matembezi hayo yatafanyika Oktoba 28, 2017 kuanzia Taasisi ya Ocean Road hadi Stesheni na wananchi wametakiwa kujitokeza  kwa wingi kuchangia damu kwa wagonjwa wenye saratani.

Akizungumza na mwandishi wa mtando huu jijini dare s salaam, Meneja Uchunguzi wa satarani na Elimu kwa Umma wa taasisi ya Ocean Road, Dkt Maguha Stephano alisema asilimia 12 ya wagonjwa wapya wanaofikishwa katika taasisi hiyo wanaumwa saratani ya matiti.

"Mwaka 2006 hadi 2015 inakadiriwa wagonjwa 6000 walipimw kati yao wagonjwa 900 wanasaratani ya matiti, "amesema Dkt Stephano.

Alisema  kwa sasa taasisi hiyo imekuwa ikipokea wasichana wenye miaka 25 wakiwa na saratani ya matiti hali inayochangiwa na vihatarishi kadhaa.

Alisema sababu za kimaumbile ni moja ya vihatarishi vya saratani, wanawake ndiyo waathirika zaidi na kwamba wanaume ni hatari zaidi.

Aidha Dk Stephano ametoa wito kwa wananchi kujitokeze kwa wingi  kushiriki katika matembezi hayo ya kuchangia damu wagonjwa wa saratani kutokana na matibabu yao kuitaji damu nyingi.

"katika matembezi hayo Kutakuwa na uchunguzi wa saratani ya matiti sambamba na uchangiaji wa damu kwa wagonjwa wa saratani kwani huwa na upungufu wa damu hasa wale wenye vidonda vinavuja damu" Alisema Dk Stephano.

Aidha Dk Stephano Aliongeza kuwa kutokana kuwepo pia na wagonjwa wenye saratani ya damu ambayo huwa na uhitaji wa damu mara kwa mara jambo linalopelekea kuhitaji damu nyingi kipindi chote cha matibabu.


No comments