Breaking News

Rais Magufuli Awaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu Na Wakuu Wa Mikoa Leo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akila kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi mara baada ya kula kiapo hicho leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti  akila kiapo cha kushika nafasi hiyo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William akila kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William akisaini hati ya kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Benjamin William mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipokutana katika hafla ya kuwaapisha Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Mikoa leo Jijini Dar es Salaam. 
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu walioapishwa pamoja na Baadhi ya Mawaziri mara baada ya hafla ya kuwaapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija - MAELEZO.

No comments