Waziri Nishati Dkt. Kalemani Awapo Onyo Watumishi Tanesco
Waziri
wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewatangazia kiama wafanyakazi wa TANESCO
nchini watakaoshirikiana na watu kuiba miundo mbinu ya umeme, ili kuhakikisha
huduma hiyo haihujumiwi kama zingine.
Dkt.
Kalemani ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na maafisa wa TANESCO, na
kusema shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa kufuatia umeme unaopotea,
kutokana na kuhujumiwa miundo mbinu yake, na wizi wa umeme uliokithiri unaofanywa
na baadhi ya wateja.
Taarifa
hiyo imetolewa baada ya TANESCO kugundua wateja zaidi ya mia moja wanatumia
umeme bila kulipia hali inayolitia hasara shirika, baada ya kufanya operesheni
maalum ya kukagua watu wanaoiba umeme jijini Dar es salaam.
Kufuatia
operesheni hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakiyakimbia makazi yao kuogopa kutiwa
mikononi mwa polisi, na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
No comments