Breaking News

Wasanii kibao Kunogesha Uzinduzi Wa Filamu Mpya Ya 'Mammu'.

Na Francis Peter
WASANII wa nyota walioalikwa katika uzinduzi wa wa filamu ya 'Mammu' wameoneka kuanzisha mipango yao ya kuona mambo Yanakwenda vema baada ya kuutangaza vilivyo huku wakipokewavyema katika akaunti zao za mitandao

Msani wa filamu na tasnia ya tamthiliya nchini Rakheem David amepanga kuwapa raha mashabiki wake katika uzinduzi wa ujio mpya wa filamu iitwayo 'Mammu'unaotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Kking D Hotel iliyopo Africa sana.

Kuhusiana na hali inayoendelea Katika mitandao ya kijamii katika akaunti hizo za mastaa hao waalikwa Rakheem alimeliambia mtandao huu jijini Dar es Salaam kuwa hadi sasa ujio huo umekuwa kivitio kwani akaunti za mastaa hao zimeonekana mara baada ya kupost kuizungumzia kumekuwa na mwitiko mkubwa kutoka kwam mashabiki kutokana na kunyesha utayali wa kuipokea filamu hiyo wakikubali mvuto wa maandalizi.

"Katika uzinduzi wangu nimejipanga kwa watakao fika watapita
kwenye Red Carpet sambamba na kufanya mahojiano nakuwa usiku wa uzinduzi umeandaliwa na Afrocinema Tours Campany chini ya Richard Kabisi,"alisema Raheem.
Aidha Nyota huyo ambaye tayari ni mwenye umaarufu  awali
amewahi kufanya vema katika filamu kama iliyoitwa 'kibajaji
iliyoshirikisha nyota wengine kama Motorola, Irene Poul pamoja na nyingine iliyoitwa 'Mama Ntilie 'iliyoshirikisha nyota kama Gabon, King Majuto pamoja na Irene Poul.

Rakheem ameweza kufanya kweli pia kupitia tamthiliya ya Duty
inayooneshwa kupitia Star Tv kila siku za jumatano saa 1:00 usiku.

Ukumbi huo umeandaa uzinduzi huo kupitia mpango mpya uitwao 'New Bambaz Launch' utakao wakutanisha wasanii  wanao tikisa kwa kazinzuri , ambapo kila Ijumaa itakuwani kawaida kwa msanii wa Bongo Flavour au filamu inayobamba kufanya makamuzi.

No comments