Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Afrika Wa Bima Ya Maisha 2017
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano wa Afrika wa Bima ya Maisha, Khamis Suleiman
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano habari
Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu Kassim Majariwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kikao cha semina ya
umoja wa makampuni ya bima afrika (AIC).
Akizungumza
na waandishi wa habari Mapema leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kamati ya
maandalizi Bw. Khamisi Sulemani alisema semina hiyo itafanyika mjini Arusha
katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC).
Alisema
semina hiyo inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 1 hadi 3 hivyo
wananachi wanataweza kuhudhuria fursa hiyo ili kutambua umuhumi
wa mwananchi kuwa bima.
Alisema nchi
za Afrika bado kuna changamoto kwa wananchi kuhusu matumizi ya bima ambapo
takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 0.7 ya wananchi wa Tanzania ndiyo wanaotumia
bima, wakati nchini kenya asilimia 2.5, na Uganda asilimia 0.5.
“Swala
la matumizi ya bima bado ni changmoto hasa kwa nchi nyingi za afrika
hivyo jitihada zaidi zinaitajika kuhakikisha wananachi wanapewa elimu juu ya faida
ya matumizi ya mifuko hiyo” Alisema Bw. Sulemani.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa Afrika wa Bima ya Maisha,
Magreth Ikongo akizungumza na waandishi wa habari.
Aidha Bw. Sulemani
aliongeza kuwa “Kuna nchi zaidi ya 20
zitashiriki katika mkutano huu na mada zitakazozungumziwa ni pamoja na zile
zitakazosaidia mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutakuwa na dama za
bima kuangalia wapi tulipo na wapi tunapotaka kwenda,
“Azma yetu
ni kuleta msisimko kwa wananchi husasi kwa wananchi kununua kiwango kikubwa cha
bima kuliko ilivyo sasa hivi kwa kuongeza mteja mmoja mmoja na kuongeza mapato
kwa taifa,” amesema Seleima.
Aidha Suleimani
amesema mkutano huo utatumika kusaidia kukuza sekta ya utalii, “Tumeona hii ni fursa ya
kipekee kuendeleza soko letu la utalii na ndiyo maana tumeamua kufanya mkutano
huu Arusha na kutakuwa na siku moja ya kuwapa fursa wajumbe kuweza kutembelea
vituo vya utalii.
Kwa upande wake mjumbe
wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa afrika wa bima ya maisha, Magreth Ikongo ametoa
wito kwa makampuni yanayojihusisha na bima nchini kutumia fursa hiyo kutatua
changamoto wanazoweza kumbana nazo.
Pia amewataka
wananachi kujiokeza kwa wingi kuhudhuria kwenye semina hiyo ili luweza kujua
dhana ya serikali kuwekwa msisitizo katika bima.
Semina
hiyo ambayo imebeba kaulimbiu isemayo Mchango
Sekta Ya Bima Katika Mapinduzi Ya Viwanda Na Maendeleo Endelevu.
No comments