Naibu Waziri Uchukuzi Na Mawasiliano Mhandisi Nditiye Waliojenga Makazi Katika Miundombinu Ya Reli Wavunje Nyumba Zao.
Naibu Waziri wa ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Atashasta Nditiye, akieleza jambo mbele ya baadhi ya viongozi wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosa akifafanua jambo mbele ya Naibu
Waziri Atashasta Nditiye.
Wafanyakazi kutoka vitengo mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Atashasta Nditiye (hayupo pichani).
Dar es salaam:
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewataka wananchi waliovamia na kujenga
makazi katika maeneo ya miundombinu ya Reli kubomoa nyumba zao kwa hiari
yao kabla serikali haijawasaidia kufanya hivyo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Atashasta Nditiye alipotembelea Kampuni ya Reli Tanzania
(TRL) na kuelezwa kuwa imeanza kuboresha miundombinu kwa ajili ya kurejesha
safari za treni kutoka Tanga kuelekea Kilimanjaro hadi Arusha.
“Kwa hiyo wale ambao wamevamia maeneo ya reli
wabomoe wengine, vinginevyo tutawasaidia na hata fidia ikibini ya kuwabomolea
tutawadai,” amesema.
Aidha amesema kwa wale ambao walikuwa wamejenga kwa
vibali harali na kufuatwa na miundombinu ya reli watalipwa fidia lakini kwa
waliovamia hawatalipwa.
Amewataka wananchi katika maeneo yote nchini ambayo
reli inapita kuhakikisha wanapisha ili ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard
Gauge ufanyike bila vikwazo na kukamilika mapema.
Kwa upende mwingine amewataka watumishi wa TRL
kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili
kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri kwa usafiri wa njia ya reli kwani
atakayekwenda kinyume serikali haitamvumilia itamchukulia hatua za kisheria.
Akizungumzia kuhusu kuboreshwa kwa reli ya kutoka
Tanga kuelekea Kilimanjao hadi Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja
Kadogosa, amesema maboresho hayo wameanzia Korogwa na sasa wamesakarabati
kilometa 20 hadi Mombo na lengo ni kuanzia mwakani treni zianze safari
kupitia reli hiyo.
Aidha amesema kinachowasukuma kufanya maboresho
hayo ni kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusafirisha
abiria na mizigo nchini.
Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge
amesema hadi sasa maendeleo ya ujenzi huo ni mazuri na kwamba wamekwisha fanya
usanifu na wemeanza ujenzi wa matuta pamoja na kambi.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa TRL Focua
Sahani amemweleza Naibu waziri kuwa Kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto ya
upungufu wa wafanyakazi, wanahitaji vichwa visivyopungua 45 na kuboresha
mabehewa 17.
No comments