Breaking News

Mhe. Amina Shaban: Awataka Wahitimu Wa Chuo Cha PSPTB Kuacha Kupokea Rushwa.

Amina Khamis Shaaban (aliyemwakilisha Dkt Ashatu Kijaji) akiongea na wahitimu wakati wa mahafari ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam
Kutoka (kulia),Bw Ismail mwita ambaye ni mjumbe wa bodi wa PSPTB akiwa ni mmoja wawaliopewa cheti kutokana na mgeni rasmi (wa tatu kutoka kulia) wakati wa mahafari ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam. 

Wahitimu wa Ngazi ya cheti cha msingi wapatao 23 ambao kwa pamoja wamesimama baada ya kutunukiwa wakati wa mahafari ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam.  
 Wahitimu wa Ngazi ya cheti wapatao 280 wakiwa wamesemama mara baada ya kutunukiwa wakati wa mahafari ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam

Ndugu na jamaa wa wahitimu waliofika kuwasindikiza ndugu zao waliohitimu elimu ya ununuzi na ugavi katika mahafari ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam.  

Picha ya pamoja mgeni rasmi, Viongozi wa bodi na  Wahitimu katika mahafali ya chuo cha PSPTB yaliyofanyika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam.  

Dar es salaam:
Wahitimu wa ngazi mbalimbali katika fani ya manunuzi na ugavi wametakiwa kujiepusha vitendo vya kuomba na kupokea rushwa pindi watekelezapo wajibu wao hili kusaidia serikali kuepuka mzigo wa hasara kubwa ambayo imekuwa wakipata kufatia baadhi yao kujiusisha na vitendo hivyo.

Akifungua sherehe za mahafari hayo, mwenyekiti wa bodi ya ununuzi na ugavi Sr. Dkt. Hellen Bandiho alisema bodi itaendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini ambapo kati ya watahiniwa 3086 waliofanya mitihani, 1,101 wamefaulu.

"kutokana na mtaala wa bodi kutambulika na kuthibitishwa na taasisi ya kimataifa ya IFPSM, wahitimubwa leo wa ngazi ya CPSP watatunukiwa vyeti viwili,  yaani cheti chetu cha CPSP na cha IFPSM. Hii ni hatua kubwa katika kuwatambulisha wahitimu wetu katika soko ajira kimataifa". Alisema Sr. Dkt. Hellen Bandiho


Pia ametanabaisha kuwa wakati bodi hiyo uwapa miongozo ya maadili ya kitaaluma kwa kushirikiana na vyuo vya mafunzo ya juu yameimizwa kuanzishwa kwa mafunzo mapya hali inayopelekea bodi hiyo kutambulika kimataifa.


Aidha akizungumza katika mahafali hayo Mgeni rasmi Dkt Ashantu Kijaji ambaye aliwakilishwa na Mhe. Amina Khamis Shaban ameitaka bodi hiyo kusimamia mienendo ya wanataaluma ikiwemo kuchukua hatua za kuwafutia usajili wale wote wanaokiuka taratibu na mienendo ya taaluma.

“Ili kuthibiti mienendo ya kimaadili ya wataalam wenu, ni lazima watu wote wanaofanya kazi za ununuzi na ugfavi nchini, wawe wamesajiliwa na bodi kwa mujibu wa sheria” alisema Amina Shaban.

Pia amewahasa wahitimu kutumia fulsa na utaalamu wao kwa manufaa ya taifa hili kusaidia kupunguza hasara ambayo taifa limekuwa ikipata kutokana na ununuzi na ugavi, na kujiepusha wasitumie fulsa ya elimu waliyopata kwa ajili ya kuchukua rushwa ili kufanikisha ubadhirifu jambo litakalopelekea serikali kupata hasara.

Aliongeza kuwa “mtu yeyote atakayebainika kuingiza hasara au kupokea rushwa kutokana na ofisi, cheo hama nafasi aliyonayo tutamfukuza na kumfungulia mashitaka, serikali ya awamu ya tano haitamvumilia yeyote atakayefanya kosa hilo”.

Hata  hivyo amewataka wahitimu hao kujiendeleza na wasibweteke kwa elimu waliyopata ila wanatakwia kujiendeleza na kuwa wabunifu kutokana na mabadiriko ya teknolojia  na kimfumo yanayobadirika kila siku ili mambo mapya yasiwapite bila kujua.

No comments