LIPUMBA NA WENZAKE WAGONGA MWAMBA MAHAKAMANI
Mahakama
Kuu imekataa pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria wa Serikali dhidi ya
maombi ya kuizuia kufanya kazi Bodi ya Wadhamini wa CUF, kambi ya mwenyekiti
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Uamuzi
huo ulitolewa jana Alhamisi na Jaji Wilfred Dyansobera aliyetupilia mbali hoja
za pingamizi zilizotolewa na wajibu maombi wakipinga maombi yaliyofunguliwa na
Mbunge wa Malindi(CUF), Zanzibar, Ally Saleh.
Kutokana
na uamuzi huo, Mahakama itaanza kusikiliza maombi ya mbunge huyo anayeomba zuio
dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CUF ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Profesa
Lipumba.
Akizungumza
na waandishi wa habari mmoja wa mawakili wa CUF, Juma Nassoro kwa upande wa
katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif alisema Jaji Dyansobera ameamuru
usikilizwaji ufanyike kwa njia ya maandishi.
Nassoro
amesema muombaji ametakiwa kuwasilisha hoja zake Oktoba 19 na wajibu maombi
wametakiwa wawe wamezijibu ifikapo Oktoba 27.
Amesema
Jaji Dyansobera ameelekeza iwapo muombaji atakuwa na hoja za nyongeza awe
ameziwasilisha ifikapo Novemba 4 na shauri litatajwa Novemba 6.
Mbunge
Saleh alifungua maombi hayo kutokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani
hapo akipinga uhalali wa wajumbe wa bodi walioteuliwa na Profesa Lipumba.
Anaiomba
Mahakama itoe amri ya zuio la muda dhidi ya wadaiwa, wakala wao na watu wote
wanaofanya kazi kwa maagizo yao kutokujihusisha kwa namna yoyote na masuala ya
chama hicho mpaka uamuzi wa shauri lake la msingi utakapotolewa.
Wajibu
maombi ni Ofisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita),
aliyewakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wengine
ni Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, mwenyekiti wa bodi hiyo, Peter Malebo na
wajumbe wa bodi hiyo.
No comments