Breaking News

Lulu Ateuliwa Kuwa Balozi Tamasha La Kimataifa La Sinema Zetu.

Balozi wa sinema zetu, Elizabeth Michael akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), kushoto ni mwenyekiti wa tamasha hilo Profesa Martin Mhando, festival director Jacob joseph
Msimamizi wa Chaneli hiyo ambaye pia ni Mratibu wa tamasha hilo Zamaradi Nzowa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
KITUO cha Runinga cha Azam kupitia Chaneli 103 kimemteua Msanii wa maigizo nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' kuwa Balozi wa Maonyesho ya Tamasha la Kimataifa la Sinema Zetu linalotarajiwa kuanza  mwezi Januari hadi Aprili Mosi mwakani.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Msimamizi wa chaneli hiyo ambaye pia ni Mratibu wa tamasha hilo Zamaradi Nzowa wakati akiwafafanulia wanahabari kuhusu mcahakato mzima wa kupata filamu zitakazoshindanishwa.

Amesema wamemteua muigizaji huyo kuwa balozi wa tamasha hilo kutokana na kuianza sanaa hiyo siku nyingi tangu akiwa mtoto mdogo huku akibainisha lengo lake ni kutoa wigo mpana kwa wasanii wa maigizo kujitangaza kimataifa.

" Lulu ameteuliwa kuwa balozi kwa sababu ni msanii aliyeanza maigizo siku nyingi tunaamini atalitangaza tamasha tunaamini kupitia yeye watu wengi wataangalia tamasha litakalokuwa na manufaa kwa wasanii wetu," amesema Zamaradi.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa tamasha hilo Msanii Elizabeth Michael (Lulu) alisema katika tamasha hilo kutakuwa na vipengele mbalimbali vikiwemo vya Filamu bora itakayozawadiwa Sh milioni 1.5, Filamu fupi Sh milioni 1.5, Muigiaji bora wa fialmu ndefu Sh milioni tano, filamu fupi Sh milioni 1.5, Muigizaji bora wa Makala Sh milioni tano, muigizaji wa bora wa kiume na wa kike wa  filamu ndefu watazawadiwa Sh milioni tano kila mmoja.

Lulu aliongeza kuwa pia  Mchekeshaji bora atakeyapata sh milioni 2, Mwandishi bora wa filamu nddefu Sh milioni mbili na wa fupi sh milioni moja, Wahariri wa filamu ndefu Sh milioni mbili, Muingizaji mziki wa filamu ndefu sh milioni mbili wa fupi sh milioni moja.

Amezitaja zawadi nyiningine ni kwa mpiga picha bora wa filamu ndefu sh milioni mbili huku wa fupi atapata sh milioni moja, makala inayozungumza utaifa sh milioni moja pamoja na watazamaji kupata fursa ya kuchagua filamu bora itakayopata sh milioni moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo, Jacob Joseph amesema tamasha hilo litahusisha filamu 150 kutoka mikoa mbalimbali na kwamba filamu za Kiswahili kutoka Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Naye Rais wa Jopo la Majaji, Profesa Martin Mhando amesema kutakuwa na vituo vya kupokea filamu katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza na Dar huku akiongeza kuwa hakutakuwa na upendeleo katika kupitisha filamu.

Muigizaji Lulu amekishukuru kituo hicho kwa kumteua nafasi hiyo na kwamba tamasha hilo liatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia filamu.

No comments