Kauli Ya Waziri Lukuvi Mara Baada Ya Kubomoa Nyumba Yake Kupisha Upanuzi Wa Barabara
Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameshiriki zoezi la uvunjaji wa nyumba
kwa kuvunja nyumba yake kwa hiari iliyokuwa imejengwa ndani ya hifadhi ya
barabara ili kupisha upanuzi wa barabara.
Waziri Lukuvi amevunja
nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara kuu iendayo
katika hifadhi ya Ruaha katika Kijiji cha Mapogolo, mkoani Iringa.
“Kama kiongozi nimeamua
kuonyesha mfano kumuunga mkono Mhe. Magufuli ambaye ameamua kuiboresha barabara
hii kuwa kiwango cha lami mpaka Ruaha National Park ili kuongeza mapato ya nchi
lakini pia kuongeza vipato kwa wananchi wa barabara hii wanayoitumia”.
“Kwa faida hizo nimeamua
mimi mwenyewe kuvunja leo hii nyumba ili wananchi wa eneo hili ambao barabara
hii itajengwa lazima wahakikishe wanabomoa wenyewe nyumba zao,” alisema Waziri
Lukuvi.
Aidha Waziri Lukuvi
aliwataka wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara
kuzivunja wenyewe nyumba zao ili kurahisisha zoezi la upanuzi wa barabara hiyo
uwe wa muda mfupi, kwani barabara hiyo inajengwa kwa manufaa yao.
“Lazima tutii sheria bila
shuruti. Tuliowekewa alama ya X tuvunje nyumbza zetu ili kazi ya ujenzi wa
barabara hii iwe nyepesi, gharama iwe ndogo na iende kwa muda mfupi,” alisema
Waziri.
Vilevile aliwakumbusha
wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuwa
wasitegemee fidia yoyote kutoka serikalini na badala yakee waanze kuzibomoa
nyumba zao pasipo kusubiri kuja kubomolewa kwa nguvu.
“Serikali haitolipafidia
kabisa kwa watu waliojenga kwenye eneo la barabara kama mimi,” alisema.
No comments