JUKATA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI NCHI NZIMA KURUDISHA HAMASA YA WANANCHI KUSHIRIKI MICHAKATO YA KIDEMOKRASIA
Jukwaa la katiba Tanzania
(JUKATA) limeadhamia kufanya maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la
kurudisha hamasa kwa wananchi kuendelea kushiriki michakato ya kidemokrasia siku
ya tarehe 30 mwezi huu ambapo ngazi ya kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam
kuanzia ofisi za Jukata hadi viwanja vya Mnazi Mmoja.
Akisoma mbele ya
waandishi wa habari mrejesho wa maadhimio ya kikao cha bodi na mkutano mkuu wa
dharura uliofanyika tarehe 25 na 26 mwezi septemba katika ukumbi wa cathedral
social hall mkoani Dodoma mwenyekiti wa JUKATA Bw Herbron Mwakagenda alisema
tayali wameshamwandikia barua rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kuomba ayapokee maadamano hayo.
Alisema sambamba na
hitaji la kisheria pia Jukata wameshapeleka barua kwa jeshi la polisi kanda
maalum ya dar es salaam, kwa upande ya mikoa mingine nje ya dar es salaam
tayali pia wanachama wao wameshapeleka taarifa kwa wakuu wa polisi wa wilaya
kuwafahamisha njia yatakapopita maandamano hayo ya amani na kuwaomba wakuu wa
wilaya wa maeneo hayo kuyapokea.
“Maadhimio ya mkutano
mkuu ambao wanachama wote 225 kutoka Tanzania bara na Visiwani na kutokana na
maoni ya wananchi ambayo JUKATA imekuwa ikiyapokea tangu kutofanyika kura ya
maoni kupitisha katika mpya mkutano huo kwa kauli moja wameadhimia kufanya
maandamano ya amani nchi nzima hili kurudisha amasa kwa wananchi juu ya mchakato
huo” Alisema Bw Mwakagenda.
Aidha Bw Mwakagenda
aliongeza kuwa sambamba dhima ya maandamano hayo ametaja sababu kuu mbili
ambazo JUKATA wameona ni vema maandano hayo yakapokelewa na Mhe Rais kuwa ni kutambua
jitihada za Mhe Rais katika kusimamia rasilimali za madini, kupinga vita rushwa
na matumizi mabaya ya mali za umma, kwa manufaa ya wananchi wa kizazi hiki na
kijacho.
Alitaja sababu
nyingine kuwa ni kufikisha kwa Mhe Rais ujumbe wa haja ya kurejewa kwa mchakato
wa katiba mpya Tanzania ili ukamilike na kuwezesha kupatikana kwa katiba ya
wananchi hivyo kusaidia hatua ambazo amekuwa akichukua kuweza yasilete tija na
maendeleo endelevu ya muda mrefu kutokana na mengi kukosa msingi wa kkatiba.
Bw Mwakagenda pia
ametoa wito kwa wandishi na vyombo vya habari wao kama nguzo muhimu katika
jamii katika kufikisha habari na taarifa muhimu kwa taifa kuzipatia kipaumbele
habari zinazohusu masuala ya kidemokrasia hasa suala la mchakato wa katiba mpya
kwani kupitia wao wanaweza kujenga au kubomoa kwani taarifa ni moja ya silaha ambayo
inaweza kuwa na madhara makubwa kama ikipotoshwa.
Vikao vya bodi na
mkutano mkuu wa dharura ambao ulikutanisha wanachama wote 225 kutoka Tanzania na
Zanzibar mjini Dodoma, Bw.Hebron Mwakagenda alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya
wa Jukwaa la katiba na Ndugu Mussa Kombo
kutoka Zanzibar kuwa makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mitatu.
No comments