Zitto Kabwe 'Ampa Makavu' Spika Job Ndugai
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe
amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job
Ndugai na kusema kuwa anamsikitikia sana kama haoni jinsi heshima ya
Bunge inavyoshuka.
Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii
baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe
pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya
Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni.
Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati
hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai
ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala
asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha.
"Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni
heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili,
Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge
anapigwa risasi mkutano wa bunge ukiendelea wabunge wazoefu tulikuwa na
matumaini makubwa na spika Ndugai tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu
kutoka Ikulu anatuangusha angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta
unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya"
alisema Zitto Kabwe
Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa Ndugai alitamani kufikia japo
robo marehemu Sitta katika kuongoza shughuli za bunge lakini ameshindwa kufikia
hata asilimia ya Anna Makinda.
"Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba
afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 sasa
hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba aliuliza wajumbe gani
awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge" alisema Zitto Kabwe.
No comments