Mufti Yakabithi Ripoti Ya Tume Yake Kwa Waziri Lukuvi
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William
Lukuvi amekutana na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir pamoja ujumbe wake wa Tume ya
Mufti iliyoundwa kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA
zinarejeshwa.
Waziri
Lukuvi amepokea ripoti hiyo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John
Pombe Magufuli la kumtaka Waziri Ardhi afuatilie kwa makini maeneo yote ya
waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na
yaliyomilikishwa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi.
Katika ujumbe huu Mufti ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA
Mwalimu Salim Abeid, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko, Makamu
mwenyekiti wa Tume ya Mufti na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman
Issa na Katibu wa Tume ya Mufti Alhaj Omary Igge.
Baada ya kukabithi ripoti hii Mufti Sheikh Abubakar Zubeir
amemshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William
Lukuvi kwa kupokea Ujumbe wake wa Tume ya Mufti na kumuomba achunguze na
kuchambua kwa makini maeneo yote ya Bakwata yanayohusiana na migogoro ya ardhi.
Tume hii ya Mufti ya Kuhusu urejeshaji wa mali za waislam iliundwa
na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kukukutana Mheshimiwa Rais na
kumuomba awasaidie kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA
zinarejeshwa BAKWATA.
Mara baada ya kupokea ripoti hii Waziri Lukuvi amemuahidi Mufti
Sheikh Abubakar Zubeir kwamba atatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa Rais na
ataifanya kazi hii katika muda mfupi ujao na kusimamia kikamilifu kwa kufuata
sheria.
No comments