Breaking News

Tgnp Kuwakutanisha Wanaharakati Na Watetezi Wa Haki Za Wanawake Katika Tamasha La 14 La Jinsia Sept 5 Jijini Dar.

Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya Tgnp, Vicensia Shule (Kushoto) Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Leo Kuzungumzia Tamasha La Jinsia La Mwaka 2017 Linalotarajia Kuanza Rasmi Septemba 5 Hadi 8 Ya Mwaka 2017 Katika Viwanja Vya Tgnp Mabibo Jijini Dar Es Salaam

Dar es salaam
Mtanadao wa kijinsia (TGNP) Kwa kushirikiana Na Asasi Za Kiraia Umeandaa Tamasha la kijinsia litakalowakutanisha pamoja wanaharakati, watu binafsi, vikundi Kutoka Ndani Na Nje Ya Nchi kuanzia Septemba 5 Hadi  8 Ili  Kuwajengea Uwezo Wanawake Katika Masuala Ya Usawa Wa Kijinsia.

Akizungumza Jijini Dar Es Salaam  Mwenyekiti Wa Bodi Ya Tgnp Mtandao Bi.Vicensia Shule Amesema Kuwa Tamasha Hilo Ni La 14  Tangu Kuanzishwa Kwake Mwaka 1996 Ambapo Mwaka Huu Malengo Ni Kuangalia Mafanikio Na Changamoto Zinazowakabili Wanawake.

Alisema kumekuwepo na Mifumo  Kandamizi Katika Nyanja Zote Za Maisha jambo ambalo limekuwa likipelekea kumyima Mwanamke Haki Stahiki Za Kiuchumi, sambamba Na Kunufaika Na Rasilimali Kama Sehemu Ya Jamii.

“Kumekuwepo na mifumo kandamizi ya kijamii kama vile ukatili wa kijinsia  kwa watoto wa kike huku takwimu zikionyesha kuwa Katika  Wanawake Kumi, Wanne  Wamewahi Kunyanyaswa Na Asilimia 20 Wamefanyiwa Ukatili Wa Kijinsia Katika Maisha Yao” Alisema Bi Vicensia.

Bi Vicensia aliongeza kuwa kupitia tamasha hilo washiriki watabadilishana uzoefu, kujengeana uwezo, kutafakari changamoto mbalimbali pamoja na kusherekea mafanikio yakiopatikana katika usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi wa TGNP Mandao Bi Liliani LIundi akifafanua jambo kuhusu tamasha La Jinsia La Mwaka 2017 Linalotarajia Kuanza Rasmi Sept 5 Hadi 8 Ya Mwaka 2017 Katika Viwanja Vya Tgnp Mabibo Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumiza kuhusu nafasi za uongozi kwa wanawake Alisema kukosekana kwa Miongozo katika Vyama Ya Viwango Vya Uwakilishi Kwa Jinsia ni moja ya kikwazo na Akibainisha Kuwa Mfumo Uliopo wa Kila Chama Kuwa na Utaratibu Wake Wa Kupendekeza Wagombea pasipo na Uwazi.

Aidha Bi Vicensia Ametaja Malengo Makuu Ya Tamasha Hilo Kwa Mwaka Huu Kuwa Ni Kutafakari Na Kusherehekea Mafanikio, Changamoto Zilizopo Katika Kuendeleza Usawa Wa Kijinsia, Wakizingatia Utekelezaji Wa Mikataba, Maazimio, Sera Na Mikakati Mbalimbali Ya Kimataifa, Kikanda Na Kitaifa.

Mengine Ni Kutathimini Ushiriki Wa Wanawake Katika Michakato Ya Kufanya Maamuzi Katika Uongozi Wa Kisiasa Kwenye Serikali Za Mitaaa. Kufuatilia, Kuhifadhi, Kutambua Na Kusherehekea Viongozi Wanawake Wenye Michango Ya Kuigwa Juu Ya Usawa Wa Kijinsia Na Uwezo Wa Wanawake, Hususani Mapambano Dhidi Ya Mfumo Dume Na Uliberali Mamboleo.

Pia Imo Kuimarisha Harakati Za Ukombozi Wa Wanawake Kimapinduzi Kupitia Ujenzi Wa Nguvu Za Pamoja.

Tamasha la mwaka huu limebeba ujumbe wa “Mageuzi Ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa Wa Kijinsia Na Maendeleo Endelevu

No comments