Breaking News

Prof Lipumba:Sina Mpango Wa Kupunguza Wabunge, Madiwani Wa Chama Nasimamia Katiba Ya Chama.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wabunge wateule na vingozi wa chama hicho kuheshimu katiba ya chama hicho hili kuweza kujenga chama kwa misingi ya haki sawa kwa wote sambamba na kuheshimu haki za binadamu.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es salaam katika halfa ya kuwapokea wabunge wateule wa viti maalum wa Chama hicho alisema kamwe hatasita kuchukua hatua kwa mwanachama au kiongozi yeyote atakaekiuka katiba ya chama hicho.

“Katika kuhakikisha chama kinalejea katika misingi yake ya kuanzishwa kwake sitamvumilia yeyote ambaye atakiuka katiba ya chama japo kuna watu wanazani hatua hizi nazochukua zimelenga kupunguza wabunge na madiwani wa chama” Alisema Prof Lipumba.
Alisema chama cha wananchi CUF tangu kuasisiwa kwake kimekuwa chama ambacho kimejikita zaidi katika misingi ya haki usawa kwa wote hivyo wataendelea kuikosoa serikali kwa kuzingatia haki usawa kwa wote.
Aidha Prof Lipumba amewataka wabunge hao wateule wa chama hicho kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kulinda ubadhilifu wa asilimali za nchi hususani madini.
Mapema akimkaribisha mwenyekiti wa chama Kaimu mkuu wa kitengo cha habari wa chama hicho Bw. Abdul Kambaya alisema kumekuwepo na tasisi na vikundi vya watu juu ya mgogoro unaendelea katika chama hicho mapoja na kuapishwa kwa wabunge wapya kuwa kitendo hicho cha kuwaapisha wabunge hao ni batili kutokana na mashauri yaliopo mahakamani.
“Kumekuwepo tasisi ambazo zimekuwa zikiacha kazi zake za msingi na kuanza kupotosha juu ya kuapishwa kwa wabunge wetu kutokana na kuwepo na mashauri mahakamani nazitaka kufanya kazi zao kwa madhumini ya kuanzishwa kwake badala ya kuwa tawi la chama Fulani cha siasa jambo ambalo ni kinyume na katiba zao” Alisema Kambaya.

Kwa upande wao wabunge wateule wamewakikishia viongozi na wanachama wa chama cha wananchi CUF kuwa watafanya kazi ya kukijenga chama hicho kwa ufanisi mkubwa kwa haki na usawa kwa wote sambamba na kuhakikisha wanasimamia katiba ya chama hicho.

No comments