Kutoka Zanzibar: 20 Wanaswa Wakifundishana Kufanya Mapenzi Ya Jinsia Moja
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi
Hassan Nassir
***
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za
kukutwa wakifundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir amesema watu
hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao
yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative.
Hata
hivyo hatua hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya kauli ya mkuu wa mkoa huo ambaye
pia ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama RC Ayoub Mahamoud kutamka kukomesha
vitendo hivyo mara moja ambavyo vinaharibu sifa ya mkoa huo.
Mbali
na hilo mkuu huyo wa mkoa akiliongoza Jeshi la Polisi tayari yuko katika
operesheni ya kuzidhibiti biashara ya dawa za kulevya, ambapo zaidi ya Vijana
50 mkoani humo walikubali kuachana na matumizi ya dawa hizo.
No comments