Kufatia Kuapishwa Wabunge 7 Wa Cuf Bungeni Jana Huu Ndio Msimamo Wa Kambi Ya Maalim Seif
Chama Cha Wananchi CUF Upande Unaomuunga Mkono Katibu Mkuu Wa Chama
Hicho, Maalim SEIF SHARIF HAMAD Kimesema Hakiwatambui Wabunge Wanane
Walioapishwa Jana Mkoani DODOMA.
Akizungumza Jijini Dar Es Salaam Kaimu
Mkurugenzi Wa Habari wa CUF Bw.MBARARA MAHARAGANDE Alisema Kitendo Cha
Kuapishwa Kwa Wafuasi Hao Kimefanyika Haraka Bila Kuzingatia Utaratibu.
Alisema Michakato wa Kuapishwa Kwa
Wabunge Hao Wapya ulipaswa Kusubiri Hatma Ya mashauri ya msingi yaliopo
Mahakamani hivyo kumtaka Spika bunge mhe Job Ndugai Kujitathmini kutokana
na unyeti wa nafasi yake ya kuongoza chombo hicho nyeti katika kutunga sheria
na kuisimamia serikali kufatia kitendo cha kuwaapisha wabunge hao tayali Amepoteza
Sifa kukiongoza chombe hicho.
Kwa upande wake Wakili wa chama cha CUF Bw. HASHIM
MZIRAY Alibainisha kuwa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Inaongozwa Na Katiba
Hivyo Maamuzi Ya Kuondolewa Yanaweza Kukatiwa Rufaa.
Akizungumza kwa niaba ya Wabunge Waliovuliwa
Uanachama Bi.RIZIKI SHAHARI Alisema Wataendelea Kupigania Demokrasia Na
Kuzitaka Taasisi Za Serikali kuacha kuingilia mambo ya ndan ya vyama vya siasa
pamoja na kutumika Kuhujumu Vyama Vya Upinzani.
Chama Cha Wananchi (CUF) Kimekuwapo Katika
Mgogoro Wa Muda Mrefu kati ya Katibu Mkuu Maalim SEIF SHARIF HAMAD Na Profesa
IBRAHIM LIPUMBA Ambao Umesababisha Kufunguliwa Kwa Mashauri Mbalimbali
Yanayoendelea Mahakamani kuu jijini dar es salaam.
No comments