Yaliyojiri Siku Ya Pili Kwenye Tamasha La Jinsia Mwaka 2017 Jijini Dar
Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bengi Issa
akiwasilisha Mada katika Tamasha la Jinsia 2017.
Tamasha la 14 la Jinsia mwaka
2017 lilirotaribiwa na TGNP Mtandao na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI)
limeendelea leo Jumatano Septemba 6,2017 katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo
Jijini Dar.
Tamasha hilo limeanza
Septemba 5 litaendelea hadi Septemba 8,2017, linaongozwa na mada “ Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa wa
Kijinsia na Maendeleo Endelevu”.
Tamasha la Jinsia mwaka 2017
limefunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
na linahudhuriwa na wanawake zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Mtandao Bi Liliani
Liundi Akifafanua jambo katika tamasha Tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017 leo
Jumatano Septemba 6, 2017 katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar.
Mbunge wa jimbo la
bunda mhe Esther Bulaya akichangia mada katika tamasha hilo
Mratibu
wa Masuala ya Ujumuishwaji kutoka shirika la Sight Savers Angela Michael
akiwasilisha dada katika tamasha hilo.
Siti
Abbas Ali kutoka Shirika la Zanzibar Coalition akichangia mada ambapo
amesema wanamke wa Zanzibar wanakumbwa na changamoto katika
kuchagua na kuchaguliwa ngazi za uongozi.
Baadhi ya Viongozi
Wanawake akiwemo aliyekuwa Spika wa Bunge Anna Makinda, Esther Bulaya wa
pili kutoka Kulia wakieleza jinsi walivyodhubutu kama wanawake ni katika
majadiliano ambayo yameandaliwa na TGNP Mtandao
katika tamasha hilo
la Jinsia 2017.
Mkurugenzi
Idara ya Kuondoa Umaskini Wizara ya Fedha na Mipango Anna Mwasha
akiwasilisha mada ambapo amewataka Watanzania wakiwemo akina mama kuunda
vikundi mbalimbali ili kupewa mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Mratibu
wa Ardhi kutoka Shirika la Care International Marry Ndaro akiwasilisha
mada ambapo amezungumzia masuala ya umiliki wa ardhi kwa wanawake sera
inapaswa kutoa kipaumbele kwa mwanamke ili aweze kumiliki ardhi.
Washiriki katika tamasha hilo
No comments