‘ALLAH AKBAR’ YASABABISHA NDEGE KUCHELEWA KUONDOKA AIRPORT
Abiria tisa
wamezua taharuki kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Zaventem, nchini
Ubelgiji baada ya mmoja wao kutamka matamshi yaliyosikika ‘Allah Akbar’ kwa
sauti kubwa mara kadhaa.
Watu hao tisa walitolewa na maaskari
kwenye ndege ya shirika la Ryanair, na kuamriwa mizigo yao kutolewa kwenye
ndege ili kukaguliwa zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya ndegehiyo kuondoka.
Ndege hiyo
ililazimika kuchelewa kwa masaa manne ikipisha ukaguzi wa mizigo ya watu hao,
ambao walitambuliwa kuwa ni raia wa Ubelgiji.
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka Ubelgiji wanasema abiria walioshuhudia tukio hilo wamesema
lilitokea baada ya ndege hiyo kuchelewa masaa matatu kuruka na ndipo mtu huyo
akaanza utani akitamka ‘Allah Akbar’ huku akicheka.
Hata hivyo
abiria hao nane walirudishwa kwenye ndege baada ya ukaguzi kufanyika na ndege
kuendelea na safari yake, ingawaje mpaka sasa bado haijawekwa wazi sababu za
kupekuliwa kwa watu hao kwa mara ya pili huku mitandao mingi duniani ikiandika
kuwa ni hofu ya ugaidi iliyotanda nchini Ubelgiji.
No comments