Breaking News

Breaking News: Tundu Lissu Apigwa Risasi Dodoma

Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)Tundu Lissu anadiwa kupigwa risasi akiwa Dodoma kisha kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.


Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Image result for tundu lissu
Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.
Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo zenye damu

No comments