Bonanza La Michezo Chuo Cha Kitm Lafana Jijini Dar
Meneja wa Benki ya
NMB Bi. Janeth Shango ambae ndiye mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa
bonanza la michezo lililondalia na chuo cha Kilimanjaro institute of Technology
andabusiness Management katika viwanja vya shule ya mapambano jijini Dar es salaam.
Rais wa serikali ya
wanafunzi wa chuo hicho bw. Fredrick Semiono akifafanua jambo katika ufunguzi
wa bonanza la michezo lililondalia na chuo cha Kilimanjaro institute of
Technology andabusiness Management katika viwanja vya shule ya mapambano jijini
Dar es salaam.
Waziri mkuu wa
serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro institute of Technology
andabusiness Management Bw. hilal alum akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi
wa bonanza la michezo lililondalia na chuo cha Kilimanjaro institute of
Technology andabusiness Management katika viwanja vya shule ya mapambano jijini
Dar es salaam.
Mgeni rasmi Meneja wa
Benki ya NMB Bi. Janeth Shango akikagua timu za mpira wa miguu tayali kwa
kuanza kwa mchezo kati ya wanafunzi na walimu wa chuo hicho.
Dar es salaam
Wito umetolewa kwa
wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini kutoa kipaumbele katika
maswala ya michezo pamoja na kuwa ni burudani pia michezo ni afya pamoja na
nyenzo muhimu katika kuwafanya wanafunzi hao kufatilia masomo yao.
Akizungumza wakati ufunguzi
wa bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo cha kilimanjalo Institute of
Technology jijini dar es salaam, Meneja wa Benki ya NMB Bi. Janeth Shango alisema
michezo ni afya pia michezo burudani hivyo kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu
kuendelea kutenga mda wao baada ya ratiba za masomo kwa ajili ya kushiriki
katika michezo.
Alisema benk ya NMB
kwa kutambua umuhimu wa michezo wameona ni jambo jema kujumuika katika bonanza
hilo kwani wanafunzi ambao wanajihusha na maswala ya michezo mara nyingi
wanakuwa ni watu wenye furaha na wenye afya nzuri na kuzuia magonjwa.
Bi Shango Aliongeza
kuwa kupitia bonanza hilo ambapo michezo mbalimbali itachezwa na kuwakutanisha
wanafunzi na walimu wa chuo hicho katika michezo mbalimbali inaonyesha namna
chuo hicho kilivyo na mahusino mazuri kati ya wananfunzi na walimu.
Kwa upande wake Rais
wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho bw. Fredrick Semiono alisema lengo kubwa
la kuandaa bonanza hilo nikuwakutanisha wanafunzi na walimu wa chuo hicho
katika kushiriki michezo sambamba na kuboresha mahusiano kati yao kupitia
michezo.
Alisema jumla ya timu
nne kutoka katika fani mbalimbali zitachuana vikali katika michezo ya mpira wa
miguu ambapo fainali ya itafanyika siku ya terehe 9 mwezi huu katika fukwe za
Hoteli ya Jangwani sea Breez jijini dare s salaam na washindi kukabidhiwa
zawadi zao.
Amezita timu ambazo
zinashiriki katika bonanza hilo kuwa ni timu ya Accounting, Information
Technoloy, Diploma Of Bussiness manegment na Diploma of PS ambapo shindig wa
kwanza katika mashindano hayo atajinyakulia fedha taslimu pamoja na kiroba cha
mchele.
No comments