Mhe Hamadi Rashidi Awataka Maalim Seif Na Lipumba Kukaa Kumaliza Mpasuko Kapitia Vikao Vya Chama Sio Mahakamani
Mwenyekiti wa Taifa wa ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akiwasili makao makuu ya chama
cha ADC jijini Dar es salaam.
Meza kuu ya viongozi mbalimbali waliofika katika maadhimisho miaka 5
tangu kuanzishwa kwa chama hicho jijini dar e s salaam.
Wafuasi wa chama cha ADC wakifatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa
ADC Mhe. Hamad Rashid Mohamed (hayupo pichani) katika maadhimisho ya miaka 5
Tangu kuanzishwa kwa chama hicho jijini Dar es salaam.
Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Taifa wa ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, ametoa rai kwa viongozi wa chama cha
wananchi CUF kukaa chini na kuangalia namna ya kutatua mpasuko unaokisibu chama
hicho kikongwe cha upinzani nchini.
Akizungumza katika kilele cha maazimisho ya miaka mitano tangu
kuanzishwa kwa chama hicho, alisema kamwe mahakama ahiwezi kuwa sehemu ya
kumaliza mpasuko huo kutokana na mahakama kazi yake ni kutoa hukumu hivyo
mgogoro huo utamalizika kwa njia vikao vya ndani vya chama.
“Ushauri
wangu wamalize matatizo yao kwa vikao na mazungumzo, mahakama haiwezi kumaliza
mgogoro bali inatoa hukumu tu, wao wamekuwa kila wanapokaa vikao ni kufukuzana,”
alisema Rashid.
Mhe
Hamadi amemtuhumu katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kuwa ndio chanzo cha mgogoro
huo kutokana na juhudi zinazoonyeshwa na Prof Lipumba za kumtaka arejee ofisi
kwake waongee wayamalize lakini amekuwa
hataki kusamehe na kuyamaliza hadi kufikia hatua ya kumuwekea chuki Profesa
Lipumba kwamba hawezi hata kumpa mkono.
alisema amekuwa mtu mbinafsi ambaye anatataka analoamuwa yeye liwe pasipo kusikiliza ushauri wa wengine, hivyo kuwaasa vingozi wa chama cha ADC kukataa viongozi wa jinsi hiyo ndani ya chama hicho.
Alisema
kufanya siasa kunahitaji mtu mwenye hekima na busara ambapo alibainisha kuwa
mwanasiasa mzuri ni yule mwenye mbinu na mikakati mizuri isiyo na vurugu.
Katika
hatua nyingne Mhe Hamadi amemtaka Maalim kuacha kueneza propaganda kuwa yeye ni
msaliti na kwamba ADC ni CCM “B” huku akibainisha kuwa Maalim ndiye msaliti
kwani haiwezekani kufanya mazungumzo na CCM peke yake bila kuwepo mashahidi
wakujua kinachozungumzwa kisha kukaa kimya.
“Niwatake
waache kukipaka matope chama chetu, lakini chama cha CUF tulikijenga kwa
gharama kubwa, kuna watu waliuawa lakini tulifukuzwa na Maalim bila hata Prof.
Lipumba kujua, watatue tu mgogoro wao na wasikipake ADC matope,” amesema.
No comments