Kanisa La EAGT Lamwomba Rais Kuingilia kati Mgogoro Wa Kiwanja Uliodumu Zaidi Ya Miaka 30.
Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Temeke limemuomba
Rais Dkt John Pombe Magufuli kuingilia mgogoro wa umiliki wa kiwanja kilichopo
kitalu D mtaa wa Everest uliodumu zaidi ya miaka 30.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Mdhamini wa Kanisa la EAGT nchini Mchungaji Christom Isack
Ngowi alisema kufuatia notisi inayowataka kuhamisha mali zote za kanisa kabla
ya kesho Agosti 21, siku ambayo Manispaa ya Temeke imepanga kubomoa eneo hilo,
kitendo ambacho waumini na viongozi wa kanisa hilo wamesema kingesubiri maamuzi
ya barua waliyomuandikia Rais Magufuli kuhusu mgogoro huo.
Alisema eneo hilo
ambalo kanisa lilianza kuomba umiliki wake tangu mwaka 1978 viongozi na waumini
wa kanisa hilo wameshangazwa na kile walichoeleza kuwa ni kutotekelezwa kwa
maagizo ya mawaziri wa zamani wa ardhi akiwemo marehemu Mustafa Nyang'anyi na
mwenzake Marcel Bujiku Komanya, ambao katika nyakati tofauti walizitaka mamlaka
kulipatia kanisa la EAGT Temeke umiliki wa eneo hilo.
“Vingozi wa kanisa
pamoja na kuchukua hatua mbalimbali kuwasiliana na mamlaka husika kumekuwepo na
sintofahamu kuhusu umiliki wake hivyo tumemwandikia barua mhe Rais Magufuli juu
ya mgogoro huu kwani ndio mtu pekee ambae anaweza kusimamia haki ambayo
tumekuwa tukifatilia kwa zaidi ya miaka 30” Alisema Mchungaji Ngowi.
Mgogoro
wa Kiwanja hicho uliibuka kufatia mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo kudai ndio
mmiliki wa eneo hilo tangu mwaka 1999.
No comments