Makamishna Wastaafu Polisi Watakiwa Kuwadhibiti Wahalifu Uraiani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Kamishna
Mstaafu Paul Chagonja wakati wa sherehe zilizoambatana na
Gwaride maalumu la kuwaaga makamishna wastaafu watatu, gwaride lililofanyika
katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao
walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa
ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu. Kulia ni Kamishna Mstaafu Hamdani Makame. (Picha
kwa hisani ya Jeshi la Polisi)
Kamishna Mstaafu Paul Chagonja akikagua gwaride maalum lililoandaliwa
kwaajili ya sherehe ya kuwaaga makamishna wastaafu watatu akiwemo kamishna
Chagonja, Kmaishna Paul Chagonja na Kamishna Kenneth Kaseke. Gwaride hilo
lilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo
wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu. (Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi)
Makamishna wastaafu Paul Chagonja (kushoto) na Hamdani makame
wakisukumwa kwenye gari na Makamishna Wasaidizi Waandamizi
sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi katika kuwaaga maofisa wakuu. Makamishna hao wamestaafu utumishi wa umma
kwa mujibu wa sheria na waliandaliwa Gwaride maalum la kuwaaga lililofanyika
katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam (Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi)
Na.
Jeshi la Polisi.
Makamishna
wastaafu wa Polisi Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke wametakiwa
kuendeleza elimu ya Polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa
Jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika maisha ya uraia baada ya kustaafu
utumishi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa wahalifu hawapati nafasi ya
kutamba hapa nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa sherehe
zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga wastaafu hao lililofanyika katika
viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao
walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa
ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.
IGP Sirro alisema
kazi waliyofanya wastaafu hao ni kubwa lakini kustaafu kwao siyo mwisho wa
kutumika katika kazi za Polisi na hivyo waendelee kuwa tayari wakati wowote kwa
kuwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikisha jamii kukabiliana na
uhalifu.
“Upolisi ni taaluma
kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na kwetu sisi tunaondelea
kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote mazuri mliyofanya na nyie
mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia kwa mawazo na milango yetu ipo
wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama” Alisema IGP Sirro
Akizungumza baada ya
kuagwa rasmi Jeshini Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa
Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza
tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.
Chagonja amesema
nidhamu ndio msingi wa Askari Polisi popote pale wafanyapo kazi zao hivyo
amewaomba kuendelea kusimamia sheria bila ya kumuonea muhali mhalifu yeyote.
Kwa upande wake Aliyekuwa
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame amewashukuru wananchi wote
hususani wa Visiwani kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote hali ambayo
imesababisha Zanzibar kuendelea kuwa shwari.
Sherehe hizo
zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama,
Mkurugenzi wa Takukuru Kamishna Valentino Mlowola, IGP Mstaafu Said Mwema, DCI
Mstaafu Robert Manumba na Kamishna Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam
Suleiman Kova pamoja na maofisa na Askari Polisi.
No comments