Breaking News

Lipumba Aikingia Kifua NEC, Amvaa Tena Maalim Seif.

MWENYEKITI wa chama cha Wananchi Taifa (CUF) anayetabulika na Ofisi ya msajili wa vyama vya Siasa Prof Ibrahim Lipumba ameikingia kifua tume ya uchaguzi (NEC) kufuatia madai ya Maalim Seif kuwa Tume hiyo imeshirikiana na Lipumba kupitisha bila utaratibu majina ya Wabunge 8 wa viti maalumu baada ya Chama hicho kuwavua ubunge 8 wa Viti maalumu waliokuwepo.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi kuu ya Buguruni Jijini Dar es salaam, Prof Lipumba alisema katika kikao cha tarehe 25/7/2015 cha baraza kuu la Uongozi la taifa ndicho kilichoteua na kupanga majina yote ya wabunge hao, na ilipofika tarehe 28/09/2015 katibu Maalim Seif ndiye aliyewasilisha orodha yote ya wabunge wa viti maalumu kwenye Tume ya Uchaguzi.

Baada ya Hatua hiyo Tume ya uchaguzi iliyatangaza majina hayo yaliyowasilishwa na Katibu mkuu Maalim Seif na kutiwa saini yake, na ndiyo majina hayo hayo yamepewa kipaumbele na Chama kwa hivi sasa.


Hata hivyo Lipumba ameendelea kumtaka Katibu mkuu huyo arejee katika Ofisi yake ya Buguruni tena bila hata ya kuomba msamaha kwa Mwenyekiti wake, ingawa atalazimika kupokea maagizo ya kiutendaji kutoka kwa Mwenyekiti wake Lipumba.

No comments