Dc Wa Ubungo Kisale Makori Amaliza Mgomo Wa Madereva Kituo Cha Simu 2000.
Mkuu wa wilaya ya
ubungo Mhe Kisale
Makori ameutaka uongozi wa kituo cha mabasi cha simu 2000
kusitisha ongezeko la tozo ambalo linawataka madereva wanaotumia kituo hicho
kulipa la shilling 1000 na badala yake waendelee kutoza shilingi 500 kama ilivyokuwa
awali.
Kauli hiyo inakuja
mara baada ya madereva wanaotumia kituo hicho cha simu 2000 kugoma kutoa huduma
za usafiri kufatia kualalamikia ongezeko hilo ambalo wamedai aliendani na hali
halisi ya kituo hicho pamoja na kutoshirikishwa katika mchakato mzima wa kuandaliwa
kwake.
“Naagiza kusitishwa
kwa mda tozo mpya ya shilingi 1000 na iendelee kutumia ya awali ya shilingi 500
na namwagiza mkurugenzi wa manispaa ya ubungo, meneja wa kituo pamoja na viongozi
wa madereva kukaa kujadiliana juu ya hili swala kwani kwa mujibu wa madai ya madereva yana hoja za msingi.
Alisema mhe Makori.
Mapema wakizungumza
kituoni hapo baadhi ya madereva walisema wameamua kugoma kufatia uongozi wa
kituo hicho kuongeza ushuru kutoa shilingi 500 hadi 1000 bila kuangalia hali
halisi ya biashara pamoja na changamoto nyingi zilizopo kituoni hapo.
“Uongozi wa kituo
hicho umeamua kupandisha ushru japo tayali unajua changamoto zilizopo kituoni
hapo ambazo tayalitulishaziainisha katika barua yetu kwa uongozi lakini
chakushangaza uongozi wa kituo hicho umekuwa wakishindwa zipatia ufumbuzi
matokeo yake wamekuja na ongezeko la bei ya ushuru kituoni hapo” Walisema
Wamezitaja changamoto
hizo kuwa ni pamoja na obovu wa barabara inayotumika kuingia na kutoka kituoni
hapo pamoja kuwepo na malalamiko kutoka kwa abiria ambao wanatumia kituo hicho
hasa nyakati za usiku kufati miundombinu ya taa kituoni hapo kutofanya kazi
hivyo kuofia usalama wao.
Alisema changamoto
nyingne ni kuwepo na utaratibu mbovu kwa wakusanya ushuru wa kituo hicho jambo
ambalo limekuwa kero na usumbufu kwa kipindi kirefu kwa madereva wanaotumia
kituokutokana na tabia zao za kuwatishia pamoja na kutorudisha chenji pale
wanapolipwa hela ya ushuru na kutakiwa kurudisha chenji.
No comments