MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA MGENI RASMI KESHO KATIKA KONGAMANO KUBWA LA AINA YAKE LA WANAWAKE WAOMBOLEZAO KITAIFA
DAR ES SALAAM:
Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho anatajiwa kufungua Kongamano kubwa
la aina yake la wanawake waombolezao kitaifa kwaajili ya kuliombea Taifa litakalofanyika
kwa muda wa siku tatu.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa kongamano hilo
Mchungaji Deborah Godfrey Malasy alisema lengo kuu la kongamano hilo ni kuwakutanisha
wanawake kutoka madhehebu mbalimbali nchini hili kuwajengea uwezo kutambua
nafasi yao katika jamii.
Alisema kupitia kongamano hilo wakimama ambao ni viongozi
kuwafundisha kutambua nafasi zao katika jamii hili wawe majasiri
katika kuongoza wengine kujiepusha na unyanyasaji wa kijinsia ili waweze
kuitumia fursa ya uongozi walizonazo hili kujikwamua kiuchumi
Aidha Mchungaji Debora aliongeza
kuwa Maudhui ya Kongamano ni "Tanzania Mpya"ambapo
watafanya maombi maalum kwajili ya kuombea vijana ili kurejesha maadili
ambayo kwasasa yameporomoka ambapo neno la Mungu litakuwa kutoka Yeremia
tisa 17 hadi 21.
Pia Mchungaji Debora ametoa kwa
serikali ya awamu ya inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kuwa
muadilifu, mchapakazi na mwenye kujali wananchi wake kwakuwa ndiye kiongozi
waliyekuwa wakimuomba Mungu awapatie.
Kongamano hilo la siku mbili linatarajiwa
kuanza kesho na kumalizika tarehe 22 Julai linakutanisha wanawake wa
madhehebu mbambali kutoka ndani na nje ya nchi
No comments