Breaking News

UKARABATI WA DARAJA LA MTO RUVU WAKAMILIKA

Kaimu Mkurugenzi wa RAHCO, Bw Masanja Kadogosa akikagua eneo hilo




Dar es Salaam
Ujenzi wa kipande cha Reli kilichovunjika kutoka Ruvu station kwenda Ruvu juction umekamilika leo rasmi kwa kuanza kuruhusu kupita kwa treni ya mizigo kwanza kwa muda wa siku mbili mpaka Jumapili kufuatia ukarabati wa kipande hicho.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa eneo hilo Kaimu Mkurugenzi wa RAHCO, Bw Masanja Kadogosa, ambapo alisema kuwa sehemu ilikuwa imeharibiwa ni kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha kwa muda mrefu hivyo ikapelekea RAHCO na TRL kusimamisha shughuli za usafirishaji kuelekea mikoa ya bara.

Aidha Bw Kadogosa ametoa pongezi kwa wafanyakazi wa shirika hilo kwa kufanya kazi kwa masaa 24 kuhakikisha kuwa eneo hilo lina kamilika na safari za treni zinaendelea kama awali.

Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkurugenzi wa TRL, Focus Makoye Sahani alisema ukarabati wa kipande hicho umechukua zaidi ya wiki moja tangu kutokea kwa itilafu hiyo tarehe 18 mwezi uliopita.


Nae Kaimu MKurugenzi wa ufundi na miundombinu RAHCO, Bw Felix Nlalio, alisema katika utafiti walioufanya unaonyesha kuwa umezudhulika kutokana na ujenzi wake kutumia teknolojia ya kizamani ambapo msingi wake upo juu sambamba na mabadiliko ya tabia ya nchi alisema na kuongeza kuwa tayari wamepanga kuanza ukarabati wa madaraja yote nchini.

No comments