RAHCO YAWATAKA WALIOJENGA PEMBENI YA NJIA YA TRENI KUVUNJA NYUMBA ZAO MARA MOJA
Kaimu Mkurugenzi wa
RAHCO, Bw Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu Mkurugenzi wa RAHCO, Bw Masanja Kadogosa akikagua eneo hilo
Dar es salaam
Kampuni hodhi ya
rasilimali za Reli (RAHCO) imewataka wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la
mradi wa Reli na wale waliowekewa alama za X kuvunja nyumba hizo mara moja.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli
(RAHCO) Bw.Masanja Kadogosa kuwa serikali imewataka wananchi kutekeleza jukumu la kuvunja hizo kwakuwa
muda walopewa ni wa kutosha.
Kadogosa alisema kuwa
kwa mujibu wa sheria ni kosa kwa
wananchi wote waliojenga ndani ya mita 30 katika eneo la reli wavunje haraka
ili kupisha mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa ya Standard Gage.
Ameongeza kusema kuwa
ujenzi huo tayari serikali kupitia RAHCO
imefanya malipo ya awali kwa mujibu wa mkataba ili ujenzi huo uanze mara moja.
Amebainisha kuwa hatua
mbalimbali za ujenzi wa mradi zimeshaanza usanifu jenga kwaajili ya kambi tatu
za kufanyia kazi ambazo zimejengwa katika maeneo ya Ilala-Shaurimoyo Dar es
salaam, Soga-Kibaha na Ngerengere iliyopo Morogoro.
Pamoja na hayo
Bw.Kadogosa amesema katika kuhakikisha unakamilika kwa wakati Rahco imekabidhi
magari nane kwa mshauri mwelekezi anbaye anasimamia mradi huo ili ukamilike kwa
wakati.
Aidha amesisitza kuhusu
kampuni za wazawa ambazo zinahitaji tenda mbalimbali katika mradi huo kuwa
tayari wapo katika hatua za mwisho za kufungua website itakayotumika katika
kutoa na kuchapisha taarifa na tenda zote za mradi na kusema hakutakuwa na upendeleo
katika tenda.
No comments