PATO LA MTANZANIA LAONGEZEKA KWA ASILIMIA 11
Na
Raymond Mushumbusi MAELEZO DODOMA
Pato
la kila mtanzania kwa mwaka 2016 limeongezeka kwa asilimia 11 kutoka shillingi
1,918,897 kwa mwaka 2015 mpaka kufikia shilling 2,131,299 kwa mwaka 2016.
Takwimu
hizi zimebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango wakati
akiwasilisha Bungeni Mjini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016 na
Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018.
Akifafanua
kuhusu ongezeko hilo Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Pato la Taifa kwa
mwaka 2016 lilifikia Shillingi million 103,744,606 kwa bei za mwaka husika na
kiasi hiki kiligawanywa kwa idadi ya watu 48,676,698 walipo Tanzania Bara na
kufanya wastani wa Pato la kila mtanzania kufikia kiasi cha Shillingi
2,131,299.
Ameeleza
kuwa kwa thamani ya Dola za Marekani, wastani wa pato la Kila mtu liliongezeka
kutoka Dola 967.5 mwaka 2015 hadi Dola 979.1 kwa mwaka 2016 ikionesha kuwa
Tanzania inaelekea kwenye kundi la Uchumi wa kati.
“Serikali
inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili tuweze kufikia Uchumi wa Kati kwa
kuongeza fursa mbalimbali za uzalishaji nchini,” alisistiza Mhe. Dkt Mpango.
Mhe.
Dkt. Phili Mpango ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuboresha shughuli za
uzalishaji wa tija katika Sekta zinazoajiri hususan katika Sekta ya Kilimo cha
mazao,Ufugaji na Uvuvi.
|
No comments