MAKOMANDO 7 WA MAREKANI WAPOTEA BAADA YA MELI YA KIVITA KUGONGWA JAPAN
Makomando saba wa kikosi cha maji cha
jeshi la Marekani wameripotiwa kupotea baada ya meli yao kugongana na meli ya
wafanyabiashara karibu na pwani ya Japan.
Kamanda wa meli hiyo maalum za
kuwaharibu maadui inayofahamika kama USS Fitzgerald aka Destroyer, aliokolewa
na kukimbizwa hospitalini kwa chopa (helicopter).
Meli hiyo iligongana na meli ya
wafanyabiashara iliyokuwa na makontena umbali wa kilometa 104 Kusini-Magharibi
mwa Yokosuka. Picha zilizopigwa kutoka juu zilionesha uharibifu mkubwa kwa meli
hiyo kutokana na tukio hilo lililotokea majira ya saa nane na nusu usiku wa
kuamkia leo, kwa muda wa Japan.
Kwa mujibu wa BBC kamanda mwingine wa
meli hiyo, Cdr Bryce Benson ameokolewa na anaendelea kupata matibabu
hospitalini lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kuhamishiwa katika
hospitali ya jeshi la Marekani iliyoko Yokosuka.
Hadi kufikia majira ya asubuhi,
taarifa zilizotolewa na maafisa wa jeshi la maji la Marekani zimeeleza kuwa
ingawa ‘Destroyer’ ilikuwa katika hatari ya kuzama, maeneo yote ya kuingilia
maji ndani ya meli hiyo tayari yameshadhibitiwa kitaalam.
No comments