ITEL MOBILE YATOA MKONO WA SIKUKUU YA EID AL FITR KWA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR
Balozi wa Simu ya
ITEL Bi Irene Uwoya akimkabidhi katibu mtendaji wa kituo cha kulelea watoto cha
CHAKUWAMA bwana Hasan Khamis msaada wa mchele, unga, sukali, mafuta ya kula na vifaa mbalimbali
vya shule kwa niaba ya watoto wa kituo hicho.
Balozi wa Simu ya
ITEL Bi Irene Uwoya akitoa zawadi kwa watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea
watoto cha CHAKUWAMA jijini dare s salaam
katibu mtendaji wakituo cha kulelea watoto
waishio katika mazingira magumu bwana Hasan Khamis akizungumza mara baada ya kupokea
msaada mapema jijini dar es salaam
Dar
es salaam
Kampuni ya itel
mobile kupitia kwa balozi wake nchini msanii wa maigizo ( Bongo movie) Bi Irene
Uwoya leo imetoa msaada kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira
magumu cha CHAKUWA kilichopo sinza jijini dar hili kuweza kusherekea vizuri sikukuu ya Eid Al Fitr.
Akizungumza katika
hafla ya kukabidhi msaada huo jijini dar es salaam mkurugenzi wa ITEL Bw, Saphon Asajile alisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na kituo hicho pamoja
na vingine ambavyo vimekuwa vikihakikisha watoto wanakuwa na furaha pamoja na
kupata mahitaji yanayostahili.
Alisema kwa kutambua
tupo katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na hiki ni kipindi cha
maandalizi ya kuelekea sikukuu ya Eid Al Fitr, wametoa msaada wa Mchele kg 100,
Mafuta ya Kula lita 30, Sukari, Unga wa sembe kg 25 pamoja na vifaa vya shule madaftari 200 na kalamu 100 hili na wao waweze kusherekea kwa furaha kama
watoto wengine.
Bw. Asajile aliongeza kuwa
msaada huo unatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wateja wao na kampuni
hiyo sambamba na kutoa wito kwa jamii kuonyesha upendo kwa watoto waishio
katika mazingira magumu nchini pamoja na kuendelea kununua simu za ITEL.
Kwa upande wake
katibu mtendaji wakituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu bwana
Hasan Khamis ameishukuru kampuni ya ITEL pamoja na Balozi wake Irene Uwoya kwa
msaada huo kwani umekuja mda muhafaka na sahihi kwao na kuwataka kuendelea na
moyo kwa kuendelea kusaidia makundi yasiyojiweza.
No comments