DIAMOND AMEPOST UJUMBE HUU.. MARA BAADA YA RAYVANNY KUNYAKUA TUZO YA BET
Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny
kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment
Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.
Kufuatia ushindi huo msanii Diamond
Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa
zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu
tena kufuatia ushindi huo.
“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania
Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu
na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”
“WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!…..
Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma
ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chukua hiyo #Wcb_Wasafi #WinningTeam!”
No comments