WAZIRI MKUU AELEZA HALI YA SUKARI NCHINI KUELEKEA MWEZI WA RAMADHAN
Mbunge Jakuh Hashim
Ayoub amemuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan
na kuna tatizo la sukari huku wananchi wakiwa na uhitaji na kwamba hivi sasa
zipo tani 100,000.
Amemweleza Majaliwa
kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha
wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.
Akijibu swali hilo
Majaliwa amesema kuhusu kupungua kwa sukari na mahitaji yake nchini kuwa
Serikali iko macho na itafanya jitihada za kupata mahitaji yote.
“Mahitaji ya sukari
nchini ni tani 420,000 lakini kwa sasa tunazalisha tani 320,000 hivyo mwaka huu
Serikali imeagiza tani 80,000 na tayari tani 35,000 zimeshaingizwa
nchini,”amesema Majaliwa.
Hata hivyo, Majaliwa
amewasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari waliyoipandisha kwani Serikali
inashirikiana nao ili kuweza kuweka mazingira rafiki kwa wananchi.
No comments