MHE NAPE: WATANZANIA HAWAWEZI KUTUELEWA, NA TUSIPOKUWA MAKINI HAWATATURUDISHA 2020
Mbunge wa Mtama, Mh
Nape Nnauye amefunguka na kusema hatua mbalimbali zilizochukulia na serikali
ikiwepo kubana matumizi, kufukuza wafanyakazi hewa, kuongezeka kwa mapato kama
hazita tafsiriliwa kwa maboresho ya huduma za jamii ni sawa na kazi bure.
Nape Nnauye alisema
hayo jana wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya Maji na kusema serikali
inapaswa kufanya mambo kwa kuwafurahisha wananchi kwa kuwapa huduma bora na si
vinginevyo.
"Serikali ya awamu
ya tano ilipoingia madarakani ilianzakuchukua hatua kadhaa za kuongeza mapato
ya serikali, ikiwa ni pamoja na kubana mianya ya wakwepa kodi lakini kupunguza
matumizi ikiwemo kupunguza safari, kupunguza sherehe na matumizi ambayo
kiukweli kwa namna nyingine yalionekana si ya lazima, ikiwemo kushughulika na
wafanyakazi hewa.
"Lakini pia kwa
takwimu tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7.2 haya yote hayatakuwa na
maana kama hayata tafsiriliwa kwenye maboresho ya huduma za jamii na hasa maji.
"Hatua hizi lengo
lake lilikuwa kuongeza uwezo wa serikali sasa kama hatua hizi zimechukuliwa na
matokeo yake ni chanya tunapaswa tuyaone kwenye ongezeko la huduma za jamii,
tusipofanya hivi hatua tulizochukua zitakuwa hazina maana hata kidogo, bajeti
iliyopita tulitenga bilioni mia tisa bajeti hii tukiwa tumesimamimia hatua
tulizochukua ambazo kiukweli zingeongeza uwezo wa Serikali tunatoka mia tisa na
kwenda mia sita, kwa vyovyote vile Watanzania hawawezi kutuelewa" alisema
Nape Nnauye
Nape Nnauye aliendelea
kusisitiza kuwa wananchi hawawezi kuielewa serikali kama hatua inazochukua
haziendi kubadilisha maisha yao ya kila siku, lakini Mbunge huyo alisema tatizo
la maji lipo katika kila jimbo nchi hii sema kinachotokea wanapishana ukubwa wa
tatizo.
"Ilani hii ya
Chama Cha Mapinduzi ndiyo mkataba wetu kati ya CCM na wananchi tusipoitekeleza
wananchi hawatoturudisha na huu ndiyo ukweli kwa sababu tuliwaahidi Mh Naibu
Spika na bahati mbaya tatizo la maji pamoja na kuwaathiri watu wote lakini
wakina mama ambao ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM ndiyo waathirika wakubwa wa
tatizo hili ndiyo maana sina mashaka kwamba serikali itasikiliza na kwenda
kuongeza pesa" alisema Nape Nnauye
No comments