WASIRA ARUDI KORTINI KUMNG’ANG’ANIA BULAYA, RUFAA YAKE ITASIKILIZWA KESHO
Mahakama
ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa
Jimbo la Bunda kesho.
Mahakama
hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne wa
jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa
sababu ya makosa yaliyofanyika kwa vile
Wakili wa Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya
kuitwa mahakamani.
Jopo
la majaji linaloongozwa na Jaji Mbarouk
Mbarouk liliahirisha usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo
yasirudiwe tena kwa kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.
Warufani
wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na Mawakili wa serikali,
Obadia Kamea na Angela Msagala.
Wakili
wa mjibu rufani wa kwanza wa Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi
iahirishwe kwa muda mfupi kutokana na umuhimu wake.
Jopo
hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na ombi
hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.
“Inasikitisha,
haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda wakati
tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi tulikuwa tayari
kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,” alisema Jaji Mbarouk.
Wakati rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato, Matwiga
Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani dhidi ya
Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG).
Wakili
Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani
kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa
sheria za uchaguzi na kanuni.
Alidai
tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana na
viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu mgombea wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha kura na taarifa ya mwisho
ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume
ya Uchaguzi ya Taifa.
No comments