MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA: AWAPA ONYO WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewazuia wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa
halmashauri zote mkoani humo kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi
watakapofikia lengo la kukusanya asilimia mia ya mapato ya ndani kabla au
ifikapo Juni 30, mwaka huu.
Akihutubia
mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat), Mkoa wa Mwanza mjini
Nansio, Ukerewe leo , Mongella ameonya kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi
ambao halmashauri zao zitashindwa kufikia malengo watakuwa wamepoteza sifa za
kuendelea kushika nyadhifa zao.
"Hata
wenyeviti na mameya ambao halmashauri zao zitakusanya chini ya asilimia mia
watasalia kwenye nafasi zao kwa sababu tu wamechaguliwa kwa kura, lakini
watakuwa wamedhihirisha udhaifu wao katika usimamizi," amesema Mongella
Amesema
hadi kufikia robo tatu ya mwaka wa fedha 2016/17, halmashauri zote nane za Mkoa
wa Mwanza zilikusanya mapato kwa asilimia 51 pekee.
"Asilimia
49 iliyosalia lazima zikusanywe ifikapo Juni 30, mwaka huu. Namna mtakavyofanya
mimi sijui. Lakini tusije tukaelewana vibaya muda huo ukifika bila makusanyo
kufikia asilimia mia moja."
Mkoa
wa Mwanza una wilaya saba za Ilemela, Nyamagana, Ukerewe, Kwimba, Magu,
Sengerema na Misungwi zenye halmashauri nane.
No comments