KAULI YA DIAMOND PLATNAMUZ BAADA YA PROFESA JAY KUMTETEA BUNGENI KUHUSU KUDAIWA KODI YA MIL 400 NA TRA
Mwimbaji
wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE
kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video
fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni.
Kwenye
video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika
TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400
kwa kiasi gani alichoingiza?‘
"Downloads
zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna
kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo
kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu
ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze
kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"
Baada
ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video
hiyo na kuandika; "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni
bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo
|
No comments