VIDEO: SPIKA JOBU NDUGAI AKIELEZEA MAANA YA NENO FALA BUNGENI
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana ameonyesha
aliumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Halima Mdee
kumwambia 'fala' bungeni na kusema hata kama mtu humpendi lakini si vyema
kumtusi matusi.
Job
Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo ilibidi
arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo ilitoa maana
kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri.
"Kwa
neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri
ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule
unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu
mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana
nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia
hivyo" alisisitiza Job Ndugai
==>Msikilize
hapo chini akiongea
No comments