UNFPA YATOA ELIMU KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU FISTULA
Waandishi
wa habari wametakiwa kujikita zaidi kuandika habari ambazo zitasaidia kuijengea
uelewa jamii juu chanzo na dalili za ugonjwa wa fistula ambao chanzo chake kikubwa
ni Uzazi usio salama.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semeni ya siku moja ya
kutokomeza fistula duniani kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwakilishi
wa shirika la umoja wa kimataifa la idadi ya ya watu duniani (UNFPA) nchini na
Dkt Hashina Begum alisema bado juhudi za pamoja zinahitajika hasa elimu kwa
jamii juu ya ugonjwa huo.
Alisema
shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wamekuwa
wakitoa elimu kwa juu ya chanzo cha ugonjwa fistula, madhara yake pamoja na matibabu
ya ugonjwa huo sambamba na njia sahihi
za kujinga na ugonjwa huo.
Dkt
Begum aliongeza katika kuakikisha wanatokemeza ugonjwa huo duniani UNFPA tayali
imeshatoa mafunzo kwa wakunga elfu nne ambayo kwa lengo la kutokomeza ugonjwa
huo sambamba na kuzuia vifo vya wanawake na watoto wakati wa uzazi pamoja na
kuwashauri wajawazito kuwa na utamaduni wa kuwahi vituo vya afya mapema ili
kupunguza tatizo hilo.
“katika kuhakikisha fistula inatokomezwa
duniani ni vema matunzo ya lishe bora yaanzie utotoni ili kusaidia ukuaji bora
wa nyonga ambayo itasaidia kuepukana na fistula ukubwani” alisema Dkt Begum
Kwa
upande wake mtoa mada kutoka chama cha wakunga Tanzania (TAMA), Bi Martha
Rimoyi alisema kwa mujibu wa takwimu zinaonyesha kuwa vifo vya wanawake
wajawazito vimeongezeka kutoka 454 hadi kufikia 556 kwa kila vizazi hai laki
moja kila mwaka.
Kwa
takwimu hizo inaonekana inatakiwa juhudi za pamoja hususani katika kutoa elimu
juu ya ugonjwa wa fistula kwa hili kusaidia jamii kutambua njia sahihi ya
kujikinga na ugonjwa huo ambao umekuwa ikiondoa utu na kusema ni wakati wa
kuirejesha heshima kwa wanawake.
Alisema
duniani kote kunakadiliwa kuwa na wanawake na wasichana wagonjwa wa fistula
milioni mbili na kila mwaka kuna wastani wa wagonjwa wapya kati ya 50,000 hadi
100,000 na wanaopata matibabu ni 20,000 pekee.
Kilele
cha siku ya Tokomeza Ugonjwa wa fistula duniani uazimishwa kila mwaka 23 mwezi
mei ambapo mwaka huu shirika la idadi ya watu duniani (UNFPA) limeandaa mafunzo
ya kutokomeza fistula duniani kwa kushirikiana na wadau wa afya CCBRT na AMREF.
c