Breaking News

TECNO MOBILE KUTANA NA WADAU WAKE NA KUBADILISHANA MAWAZO JIJINI DAR






Kampuni ya simu ya Tecno mobile Tanzania imeendelea kuwajali wateja kwa kuwapa zawadi ambapo imewapa fursa ya kuangalia sinema na kujumuika na wafanyakazi wa mbalimbali  kampuni hiyo ikiwa ni kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa zake.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na afisa mahusiano wa Tecno Mobile Bw. Eric Mkomoye katika shughuli hiyo ya Tecno kuwa kampuni hiyo imekuwa na kawaida ya kutoa zawadi ikiwa  ni sehemu ya kuwathamini  na kuonesha umuhimu wa wateja hao katika kuhakikisha kampuni inakua.

Mkomoye amewashukuru watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kununua bidhaa zao hasa toleo jipya la Tecno Camon (CX) yenye kamera nzuri ya mbele na nyuma ya Megapiexl 16 yenye uwezo mkubwa wa utunzaji kumbukumbu wa 16 Gb.


Aidha mkomoye amebainisha kuwa tukio hilo limejumuisha wafanyakazi na wateja 100 pamoja na washirika wengine wa kibiashara ambao wameburudika kwa pamoja kwa kuangalia sinema katika ukumbi wa  centuary  cinemax